{"id":584,"date":"2022-07-19T18:28:06","date_gmt":"2022-07-19T18:28:06","guid":{"rendered":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/?p=584"},"modified":"2022-07-19T18:28:06","modified_gmt":"2022-07-19T18:28:06","slug":"kilimo-bora-cha-parachichi-avocado-uzalishaji-na-masoko","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/kilimo-bora-cha-parachichi-avocado-uzalishaji-na-masoko\/","title":{"rendered":"KILIMO BORA CHA PARACHICHI (AVOCADO), UZALISHAJI NA MASOKO"},"content":{"rendered":"\n<p>Parachichi ni tunda linalotumiwa sana na watu wengi, linalotokana na mti wa mparachichi, hupatikana karibu maeneo mengi hapa Tanzania,&nbsp;&nbsp;Mikoa inayolima kwa wingi sana ni Njombe, Mbeya, Kagera&nbsp; pamoja na Kilimanjaro, Parachichi hupenda maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi na udongo wenye rutuba hasa udongo wa tifutifu.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"has-text-align-center wp-block-heading\">AINA ZA PARACHICHI.<\/h2>\n\n\n\n<p>Parachichi zipo za aina nyingi, aina zinazopatikana hapa Tanzania ni&nbsp; Hass, Fuerte,Choquette na&nbsp; Hall.&nbsp;<strong>1. Hass,<\/strong>&nbsp;yenyewe huwa na ukijani wa mbali kidogo na monekano wake huwa mweusi pale linapo iva, ganda lake huwa gumu lenye mafundo (rough skin), hupendelewa sana na watu kutokana na utamu mwingi pamoja na kuwa na soko kubwa la ndani na nje ya nchi kutokana na hukaa muda mrefu sokoni bila kuharibika.<\/p>\n\n\n<div class=\"wp-block-image\">\n<figure class=\"aligncenter size-full\"><img fetchpriority=\"high\" decoding=\"async\" width=\"640\" height=\"478\" src=\"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/parachichi2-1.png\" alt=\"\" class=\"wp-image-587\" srcset=\"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/parachichi2-1.png 640w, https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/parachichi2-1-300x224.png 300w, https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-content\/uploads\/2022\/07\/parachichi2-1-600x448.png 600w\" sizes=\"(max-width: 640px) 100vw, 640px\" \/><\/figure>\n<\/div>\n\n\n<p><strong>2. Choquette,<\/strong>&nbsp;huwa na rangi ya kijani kwa nje na pia huwa na ganda jembamba na laini lenye mafuta mengi sana kwa ndani, linaumbo la duara kama umbo la yai (oval shape). Hupendwa sana na watu kutokana na mafuta mengi lakini hukaa muda mfupi sokoni kutokana&nbsp; na tabia ya kuoza haraka inayosababishwa na ganda lake la nje kuwa jepesi.&nbsp;&nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp;&nbsp;<\/p>\n\n\n<div class=\"wp-block-image\">\n<figure class=\"aligncenter\"><a href=\"https:\/\/www.blogger.com\/blog\/post\/edit\/7501401375928537680\/4480937592925799800#\"><img decoding=\"async\" src=\"https:\/\/lh3.googleusercontent.com\/-GkvbyPGTpSY\/X3w6x9CfYmI\/AAAAAAAAAhw\/EH0BcmjcIWgpoOk-BazxrmxQ_-pctpDmwCLcBGAsYHQ\/w640-h628\/image.png\" alt=\"\"\/><\/a><\/figure>\n<\/div>\n\n\n<p><a href=\"https:\/\/www.blogger.com\/blog\/post\/edit\/7501401375928537680\/4480937592925799800#\"><\/a><\/p>\n\n\n\n<p><strong>3. Fuerte,&nbsp;<\/strong>aina hii ina rangi ya kijani na ganda lake huwa jepesi (thin) hufanana kidogo na Choquette, tofauti yake na Choquette ni umbo (shape), umbo la Fuerte ni ndefu na juu ni jembamba kidogo. mara nyingi hufaa kwa soko la ndani na hukaa muda mfupi sokoni kutokana na ganda lake kuwa laini ambapo hupelekea kuchibuka kwa haraka.&nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp;&nbsp;<\/p>\n\n\n<div class=\"wp-block-image\">\n<figure class=\"aligncenter\"><a href=\"https:\/\/www.blogger.com\/blog\/post\/edit\/7501401375928537680\/4480937592925799800#\"><img decoding=\"async\" src=\"https:\/\/lh3.googleusercontent.com\/-22pfbQrkvg0\/X3w6FdioCqI\/AAAAAAAAAho\/C0OWyORGgfghHjfaAfQ7Zi1SOuaxbO2JwCLcBGAsYHQ\/w640-h550\/image.png\" alt=\"\"\/><\/a><\/figure>\n<\/div>\n\n\n<p><a href=\"https:\/\/www.blogger.com\/blog\/post\/edit\/7501401375928537680\/4480937592925799800#\"><\/a><\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\">&nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp;&nbsp;&nbsp; NAMNA YA KUANDAA MBEGU.<\/h2>\n\n\n\n<p>&nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; Mbegu za parachichi huandaliwa kutoka kwenye tunda lenyewe lililokwisha komaa na kuiva vizuri, mbegu hutolewa kwenye tunda lake na kuanikwa juani kwa siku moja na baada ya hapo gamba la nje la mbegu hutolewa,&nbsp;<br>&nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp;Baada ya hapo mbegu hupandwa kwenye viriba vilivo andaliwa tayari, na mbegu hupandwa upande wa chini kuangalia juu, na upande wa juu huangalia chini (upside _down) , na pia ilikurahisisha uchipukaji wa mbegu mapema upande ulioanza kupasuka hushauriwa uwe kwa juu au kama mbegu itakuwa haijapasuka upande wowote hushauriwa kukatwa kwa kisu duara nusu na upande ulikatwa hugeuziwa kwa juu na kupandwa.mbegu huanza kuchipua (germinate) baada ya siku 45.&nbsp;baada ya miezi 3 mche huwa tayari kwa kupelekwa shambani.<\/p>\n\n\n<div class=\"wp-block-image\">\n<figure class=\"aligncenter\"><a href=\"https:\/\/www.blogger.com\/blog\/post\/edit\/7501401375928537680\/4480937592925799800#\"><img decoding=\"async\" src=\"https:\/\/lh3.googleusercontent.com\/-JtZvcxFxHkI\/X3xSwUleypI\/AAAAAAAAAjo\/M6ZIf2iEpSM8OxF6yFBJj6PWIrnW3-Q-QCLcBGAsYHQ\/w640-h547\/image.png\" alt=\"\"\/><\/a><\/figure>\n<\/div>\n\n\n<p>Miti ya parachichi huwa ya aina mbili (2), ya muda mrefu na ya muda mfupi.<br>ya muda mrefu&nbsp;ni ile ambayo hupandwa moja kwa moja shambani kutoka kwenye mche, huwa mirefu sana , na huchukua miaka 7 hadi 15 kufikia matunda ( kuanza kutoa matunda).&nbsp;<br>&nbsp;ya muda mfupi&nbsp;(ya kisasa) ni ile ambayo huunganishwa (grafting) kati ya mche (rootstock) na kikonyo (scion)cha mti ambacho tayari ni mkubwa au uliokwisha komaa na unatoa matunda kwa muda mrefu, aina hii huchukua muda mfupi sana kuanza kutoa matunda kuanzia miaka 2 hadi 3, kwa aina ya Hass huchukua mara nyingi huanza mwaka mmoja na nusu hadi mitatu (3) kulingana na utunzaji.<\/p>\n\n\n\n<h3 class=\"wp-block-heading\">FAIDA ZA KUUNGANISHA (GRAFTING) KWENYE MICHE YA PARACHICHI<\/h3>\n\n\n\n<ul class=\"wp-block-list\"><li>hufanya mche uweze kukua kwa haraka na kwa urahisi zaidi<\/li><li>hutoa nafasi ya kuchagua ni aina gani ya parachichi unahitaji kuzalisha kulingana na soko au upendeleo wako mwenyewe<\/li><li>huvumilia kushambuliwa na magonjwa na wadudu<\/li><li>unaweza kuzalisha parachichi kipindi ambacho sio msimu wake.<\/li><\/ul>\n\n\n\n<h2 class=\"has-text-align-center wp-block-heading\"><br>NAMNA YA UPANDAJI WA MICHE YA PARACHICHI.<\/h2>\n\n\n\n<h4 class=\"wp-block-heading\"><br><strong>Uchimbaji wa mashimo<\/strong><\/h4>\n\n\n\n<p>&nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp; &nbsp;Miche ya parachichi hupandwa kwa nafasi ya mita&nbsp; 7m kwa 7m kati ya mche na mche na mita&nbsp; 7m kwa 7m kati ya mstari na mstari shimo linatakiwa&nbsp; liwe na kina cha&nbsp; 60cm na upana wa&nbsp; 60cm kutegemea hali ya udongo. Wakati wa kuchimba shimo udongo wa juu (wenye rutuba) na ule wa chini (usio na rutuba) lazima utenganishwe wa juu unaweza kuwekwa kulia na&nbsp; wachini kushoto .<strong><\/strong><\/p>\n\n\n\n<h4 class=\"wp-block-heading\"><strong>Kufukia mashimo.<\/strong><\/h4>\n\n\n\n<p>Chukua samadi debe 1-2 changanya na udongo wa juu (ulioweka kulia) jaza mchanganyiko wa samadi na udongo ndani ya shimo hadi utengeneze mwinuko wa kitako cha 100 cm toka usawa wa ardhi,<strong><\/strong><\/p>\n\n\n\n<h4 class=\"wp-block-heading\"><strong>Kupanda miche.<\/strong><\/h4>\n\n\n\n<p>Kata mizizi inayotokeza nje ya mfuko, kabla ya kutoa, weka mche ndani ya shimo kisha chana nylon na kutoa taratibu hiyo nylon ili udongo usiachane na mizizi, ukishindilia kiasi, fukia shimo kwa udongo wa chini&nbsp; hadi kufikia sehemu inayotenganisha shina na mizizi ya mche.&nbsp;<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"has-text-align-center wp-block-heading\">UTUNZAJI WA MICHE IKIWA SHAMBANI&nbsp;<\/h2>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\">Magugu huzuia miche kukua vizuri wakati ikiwa midogo au michanga, wakati wa kupalilia hakikisha hauharibu mizizi kwa kuikata.&nbsp;<\/h2>\n\n\n\n<h2 class=\"has-text-align-center wp-block-heading\">UMWAGILIAJI WA PARACHICHI&nbsp;<\/h2>\n\n\n\n<p>Parachichi huhitaji maji ya kutosha ili uweze kukua vizuri, kuna njia nyingi za umwagiliaji kwenye miche&nbsp; ya parachichi.unaweza kumwagilia kwa kutumia ndoo au kufunga mfumo wa umwagiliaji.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image\"><a href=\"https:\/\/www.blogger.com\/blog\/post\/edit\/7501401375928537680\/4480937592925799800#\"><img decoding=\"async\" src=\"https:\/\/1.bp.blogspot.com\/-pMHI2Te9lFE\/X39hEXgxnmI\/AAAAAAAAV24\/3decAyY_aksxpdQ8O-qFW9Xx1FGkd7BOwCPcBGAsYHg\/s320\/IMG_20201007_100911_278.jpg\" alt=\"\"\/><\/a><\/figure>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image\"><a href=\"https:\/\/www.blogger.com\/blog\/post\/edit\/7501401375928537680\/4480937592925799800#\"><img decoding=\"async\" src=\"https:\/\/1.bp.blogspot.com\/-0AP_5MQsKCY\/X38eDOTO9TI\/AAAAAAAAV2s\/M-BVYk3AIAwikB1KDxoowz5wO8MJXpOIgCPcBGAsYHg\/s0\/IMG-20200813-WA0023.jpg\" alt=\"\"\/><\/a><\/figure>\n\n\n\n<p><strong>Kilimo mseto.<\/strong>Wakati miche ikiwa michanga panda mazao ya muda mfupi katikati ya mstari kama vile kunde na maharage kwani mazao haya huzuia magugu kuota&nbsp; na huongeza rutuba na thamani ya shamba.<strong><br><\/strong><strong>Kuweka matandazo (mulching).<\/strong>Nyasi (mulching) husaidia kuhifadhi maji ardhini na hupunguza uotaji wa magugu na pia ya kioza huongeza rutuba ya udongo, hakikisha shina haligusani na matandazo ili kupunguza athari za mchwa na moto.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><\/h2>\n\n\n\n<p><strong>NOTE:<\/strong>\u00a0Kwa mahitaji mbalimbali ya miche ya matunda kama vile parachichi, machungwa, chenza, ndimu, limau, passion, mapera,komamanga,papai fenes, stafeli miti ya mbao n.k inapatikana, miche yote ni ya kisasa na ni ya muda mfupi.kwa huduma ya uzalishaji, utunzaji pamoja na ushauri wa miche mbalimbali ya matunda na upatikanaji wake tunapatikana Morogoro mjini, popote ulipo pia tunakutumia.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-center\">Veronica J Joseph Bsc Horticulture<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-center\">Phone: 0766856431<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-center\">Email: veronicajj94@gmail.com<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Parachichi ni tunda linalotumiwa sana na watu wengi, linalotokana na mti wa mparachichi, hupatikana karibu maeneo mengi hapa Tanzania,&nbsp;&nbsp;Mikoa inayolima kwa wingi sana ni Njombe, Mbeya, Kagera&nbsp; pamoja na Kilimanjaro, Parachichi hupenda maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi na udongo wenye rutuba hasa udongo wa tifutifu. AINA ZA PARACHICHI. Parachichi zipo za aina nyingi,&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":585,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[49],"tags":[],"class_list":["post-584","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-agronomy","item-inner"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/584","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=584"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/584\/revisions"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/media\/585"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=584"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=584"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/greenagriculturetz.com\/new\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=584"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}