• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

KILIMO BORA CHA PARACHICHI (AVOCADO), UZALISHAJI NA MASOKO

Home / AGRONOMY / KILIMO BORA CHA PARACHICHI (AVOCADO), UZALISHAJI NA MASOKO
  • July 19, 2022

Parachichi ni tunda linalotumiwa sana na watu wengi, linalotokana na mti wa mparachichi, hupatikana karibu maeneo mengi hapa Tanzania,  Mikoa inayolima kwa wingi sana ni Njombe, Mbeya, Kagera  pamoja na Kilimanjaro, Parachichi hupenda maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi na udongo wenye rutuba hasa udongo wa tifutifu.

AINA ZA PARACHICHI.

Parachichi zipo za aina nyingi, aina zinazopatikana hapa Tanzania ni  Hass, Fuerte,Choquette na  Hall. 1. Hass, yenyewe huwa na ukijani wa mbali kidogo na monekano wake huwa mweusi pale linapo iva, ganda lake huwa gumu lenye mafundo (rough skin), hupendelewa sana na watu kutokana na utamu mwingi pamoja na kuwa na soko kubwa la ndani na nje ya nchi kutokana na hukaa muda mrefu sokoni bila kuharibika.

2. Choquette, huwa na rangi ya kijani kwa nje na pia huwa na ganda jembamba na laini lenye mafuta mengi sana kwa ndani, linaumbo la duara kama umbo la yai (oval shape). Hupendwa sana na watu kutokana na mafuta mengi lakini hukaa muda mfupi sokoni kutokana  na tabia ya kuoza haraka inayosababishwa na ganda lake la nje kuwa jepesi.                                             

3. Fuerte, aina hii ina rangi ya kijani na ganda lake huwa jepesi (thin) hufanana kidogo na Choquette, tofauti yake na Choquette ni umbo (shape), umbo la Fuerte ni ndefu na juu ni jembamba kidogo. mara nyingi hufaa kwa soko la ndani na hukaa muda mfupi sokoni kutokana na ganda lake kuwa laini ambapo hupelekea kuchibuka kwa haraka.                            

                            NAMNA YA KUANDAA MBEGU.

            Mbegu za parachichi huandaliwa kutoka kwenye tunda lenyewe lililokwisha komaa na kuiva vizuri, mbegu hutolewa kwenye tunda lake na kuanikwa juani kwa siku moja na baada ya hapo gamba la nje la mbegu hutolewa, 
             Baada ya hapo mbegu hupandwa kwenye viriba vilivo andaliwa tayari, na mbegu hupandwa upande wa chini kuangalia juu, na upande wa juu huangalia chini (upside _down) , na pia ilikurahisisha uchipukaji wa mbegu mapema upande ulioanza kupasuka hushauriwa uwe kwa juu au kama mbegu itakuwa haijapasuka upande wowote hushauriwa kukatwa kwa kisu duara nusu na upande ulikatwa hugeuziwa kwa juu na kupandwa.mbegu huanza kuchipua (germinate) baada ya siku 45. baada ya miezi 3 mche huwa tayari kwa kupelekwa shambani.

Miti ya parachichi huwa ya aina mbili (2), ya muda mrefu na ya muda mfupi.
ya muda mrefu ni ile ambayo hupandwa moja kwa moja shambani kutoka kwenye mche, huwa mirefu sana , na huchukua miaka 7 hadi 15 kufikia matunda ( kuanza kutoa matunda). 
 ya muda mfupi (ya kisasa) ni ile ambayo huunganishwa (grafting) kati ya mche (rootstock) na kikonyo (scion)cha mti ambacho tayari ni mkubwa au uliokwisha komaa na unatoa matunda kwa muda mrefu, aina hii huchukua muda mfupi sana kuanza kutoa matunda kuanzia miaka 2 hadi 3, kwa aina ya Hass huchukua mara nyingi huanza mwaka mmoja na nusu hadi mitatu (3) kulingana na utunzaji.

FAIDA ZA KUUNGANISHA (GRAFTING) KWENYE MICHE YA PARACHICHI

  • hufanya mche uweze kukua kwa haraka na kwa urahisi zaidi
  • hutoa nafasi ya kuchagua ni aina gani ya parachichi unahitaji kuzalisha kulingana na soko au upendeleo wako mwenyewe
  • huvumilia kushambuliwa na magonjwa na wadudu
  • unaweza kuzalisha parachichi kipindi ambacho sio msimu wake.


NAMNA YA UPANDAJI WA MICHE YA PARACHICHI.


Uchimbaji wa mashimo

               Miche ya parachichi hupandwa kwa nafasi ya mita  7m kwa 7m kati ya mche na mche na mita  7m kwa 7m kati ya mstari na mstari shimo linatakiwa  liwe na kina cha  60cm na upana wa  60cm kutegemea hali ya udongo. Wakati wa kuchimba shimo udongo wa juu (wenye rutuba) na ule wa chini (usio na rutuba) lazima utenganishwe wa juu unaweza kuwekwa kulia na  wachini kushoto .

Kufukia mashimo.

Chukua samadi debe 1-2 changanya na udongo wa juu (ulioweka kulia) jaza mchanganyiko wa samadi na udongo ndani ya shimo hadi utengeneze mwinuko wa kitako cha 100 cm toka usawa wa ardhi,

Kupanda miche.

Kata mizizi inayotokeza nje ya mfuko, kabla ya kutoa, weka mche ndani ya shimo kisha chana nylon na kutoa taratibu hiyo nylon ili udongo usiachane na mizizi, ukishindilia kiasi, fukia shimo kwa udongo wa chini  hadi kufikia sehemu inayotenganisha shina na mizizi ya mche. 

UTUNZAJI WA MICHE IKIWA SHAMBANI 

Magugu huzuia miche kukua vizuri wakati ikiwa midogo au michanga, wakati wa kupalilia hakikisha hauharibu mizizi kwa kuikata. 

UMWAGILIAJI WA PARACHICHI 

Parachichi huhitaji maji ya kutosha ili uweze kukua vizuri, kuna njia nyingi za umwagiliaji kwenye miche  ya parachichi.unaweza kumwagilia kwa kutumia ndoo au kufunga mfumo wa umwagiliaji.

Kilimo mseto.Wakati miche ikiwa michanga panda mazao ya muda mfupi katikati ya mstari kama vile kunde na maharage kwani mazao haya huzuia magugu kuota  na huongeza rutuba na thamani ya shamba.
Kuweka matandazo (mulching).Nyasi (mulching) husaidia kuhifadhi maji ardhini na hupunguza uotaji wa magugu na pia ya kioza huongeza rutuba ya udongo, hakikisha shina haligusani na matandazo ili kupunguza athari za mchwa na moto.

NOTE: Kwa mahitaji mbalimbali ya miche ya matunda kama vile parachichi, machungwa, chenza, ndimu, limau, passion, mapera,komamanga,papai fenes, stafeli miti ya mbao n.k inapatikana, miche yote ni ya kisasa na ni ya muda mfupi.kwa huduma ya uzalishaji, utunzaji pamoja na ushauri wa miche mbalimbali ya matunda na upatikanaji wake tunapatikana Morogoro mjini, popote ulipo pia tunakutumia.

Veronica J Joseph Bsc Horticulture

Phone: 0766856431

Email: veronicajj94@gmail.com

Share:

Previous Post
NAMNA  NZURI
Next Post
MWONGOZOWA KILIMO

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 1
  • IRRIGATION 5
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited