• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

JIFUNZE KILIMO CHA KUNDE

Home / AGRONOMY / JIFUNZE KILIMO CHA KUNDE
  • July 20, 2022

Mkulima Mama Angela Machibya akiwa shambani kwake Tanga , akivuna Choroko

UTANGULIZIKunde ni zao ambalo linaweza kulimwa kwa ajiliya chakula na bishara ni zoa lenye kiasikukubwa cha protini na majani yake yanawezakutumika kama mboga za majani.Ni zao ambalolinatoa mavuno ya Kiasi cha kilogram 500 hadi1500 kwa ekari.
HALI YA HEWA IFAAYONi zao linalostahimili ukame, Kunde hukubalivizuri katika mwinuko wa mita 0 hadi 1500kutoka usawa wa bahari.kunde huweza kulimwakatika maeneo yapatayo mvua kidogo kiasi chamilimita 500 hadi 1200 kwa mwaka.Hukuwavizuri katika joto la nyuzi 28 had 32 C

ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA KUNDE

Huweza kulimwa katika udongo usiotuamishamaji wa aina tofauti tofauti kuanzia kichangahadi mfinyazi.Zinaweza kupandwa katikaudongo usio na rutuba ya kutosha lakini hustawivizuri katika udongo wa tifutifu kichanga autifutifu mfinyanzi au  mchanganyiko wa mfinyazina kichanga wenye p.H kati ya 6 hadi 7, ni vizuri kupima udongo kwa ajili ya uhakika zaidi

MAANDALIZI YA SHAMBA LA KUPANDA KUNDE

Shamba la kunde liandaliwe mapema kablashughuli ya upandaji kuanza, Kama ni la kukatamiti mikubwa miti ikatwe mapema,Kama ni lakufyeka nyasi na miti midogo shughuli hiiifanyike mapema kabla hatua ya kulimwa kwashamba kwa kutumia trekta,Pawatilla,jembe lang’ombe au la mikono.shamba lisawazishwe nakukusanywa mabaki ya mimea au visiki namawe madogomadogo kama yapo.

MBEGU BORA ZA KUNDE

Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za kundeambazo zimegawanyika katika makundimakubwa mawili.Kunde zinazosimama na kundezinazotambaa.
BAADHI YA MBEGU BORA NA SIFA ZAKE

1.TUMAINI
Hukomaa kwa muda wa siku 75 – 90. Aina hii yakunde husambaa ina maua yenye rangi zazambarau na mbegu zake ni mviringo. Maeneoyanayoshauriwa kupanda ni yenye mwinuko wamita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Inahitajiudongo mwepesi wenye rutuba na usiotuamishamaji. Kunde hizi hutoa mazao hadi tani 3(kilogram 600 – 1500 kwa ekari)kwa hekta moja.Huvumilia virusi vya mozaiki vinavyotokana nawadudu mafuta wa kunde na bakteria. Aina hiiya kunde ilizalishwa mwaka 1992 na Kituoa chaUtafiti cha Ilonga kwa ushirikiano na Naliendele.
2.FAHARIAina hii hukomaa kwa siku kati ya 75 – 90.Mmea husambaa na maua yana rangi yazambarau. Mbegu zake ni za mviringo. Hustawimaeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500kutoka usawa wa bahari. Hutoa hadi tani 3 kwahekta moja (kilogram 600 – 1500 kwa ekari ).Huvumilia magonjwa ya CABMV na mabaka.Fahari ilitolewa mwaka 1982 na Kituo cha UtafitiIlonga kwa kushirikiana na Naliendele
 3.VULI_1Inakomaa kwa siku 55 – 65. Hukua ka kunyookana kusambaa kidogo. Mbegu zake ni nyekunduna za mviringo. Inastawi vizuri maeneo yenyemwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wabahari. Ikipataiwa matunzo mazuri huto hadi tani2 kwa hekta moja (Kilogram 450-800 kwa ekari).Vuli – 1 inavumilia CABMV, BP na BB Vuli – 1ilizalishwa mwaka 1987 kutoka kituo cha utafitiIlonga.

4.VULI_2
Inakomaa baada ya siku 65 – 70 baada yakupandwa inaota ikiwa imenyooka na kusambaakidogo. Mbegu zake zina weupe uliofifia na nimviringo. Aina hii husitawi vizuri maeneo yenyemwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wabahari. Katika matunzo mazuri aina hii huzalishahadi tani 3.5 kwa hekta moja(Kilogram 800-1200 kwa ekari) . Vuli – 2 huvumilia CABMV, BPna BB Vuli – 2 ilizalishwa mwaka 1987 kutokakituo cha utafiti Ilonga.


KUPANDA KUNDE

Kunde hupandwa mwishoni mwa msimu wamvua ili kuziepusha kukauka wakati mvuainaendelea kunyesha.na pia unweza kupandawakati zao jingine linakaribia kuvunwa au katikashamba lilivunwampunga na lina unyevu wakutosha.Muda mzuri wa kupanda kunde niakuanzia mwezi Februari mwishoni hadi Machina Aprili kwa maeneo ambayo mvua huchelewakuisha.  KUMBUKA; Mbegu zinazotambaa zakunde zipandwe miezi miwili kabla ya mvuakuisha kwani hizi huchukua siku nyingi kukomaana Mbegu zinazosimama zipandwe mwezimmoja kabla ya mvua kuisha.Kunde huitaji kiasi cha kilogram 4-12 za mbegukwa ekari.kiasi cha mbegu kitategemea ukubwawa mbegu,(mbegu kubwa zitahitajika kilogramnyingi) nafasi za upandaji,Ukipanda karibukaribu na mbegu itahitajika nyingi,Ubora wambegu katika uhotaji.Zisizoota vizuri huitajimbegu nyingi zaidi


NAFASI YA UPANDAJI

Unaweza kutumia nafasi zifuatazo kwa kupandakunde zakoKUNDE ZINASOSIMAMA-Tumia sentimeta 45hadi 50 mstari hadi msatari na sentimeta 15 hadi20 shina hadi shina katika mstari / Sm ( 50 X20 )
KUNDE ZINAZOSAMBAA-Tumia nafasi ya Sentimeta 70 hadi 75 mstari hadi mstari Kwa sentimeta 25 hadi 30 shina hadi shina katika mstari / Sm ( 75 X 30 )Panda kwa kufikia kiasi cha sentimeta 2.5 hadi 5ardhini na tumia mbegu tatu kwa kila shimo nabaadaye punguza uache 2 kwa kila shimo kamaunauhakika wa mbegu zako unaweza kupandamoja kwa moja mbili mbili kwa shimo

PALIZI NA KUPUNGUZA MIMEA      KATIKAMISTARI

Palilia na Punguza mimea mapema katikashamba lako la kunde.ili ikuwe ikiwa na afyabora.

MBOLEA YA SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI

Kama shamba lako halina rutuba ya kutoshaunaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tanokwa ekari moja na uhakikishe mbolea hiiimemwagiwa au imenyeshewa na mvua yakutosha kuiozesha kabla ya kupanda kundezako na pia unaweza kupanda kwa kutumiambolea ya TSP kiasi cha Kg 50 kwa ekari nabaadaye kukuzia mbolea ya SA kiasi cha Kg 50kwa ekari.

WADUDU NA MAGONJWA KUNDEKUDHIBITI WADUDU WAHARIBIFU WA KUNDE

Wadudu waharibifu wa zao la Kunde wako katikamakundi mawili:-     1. Kundi la kwanza ni la wadudu
wanaoshambulia mimea ikiwa shambani.
 Inamaana mmea hushambuliwa baada ya kuonahali inapokomaa na kutoa mbegu. Kundi lawadudu hawa lina tabia ya kufyonza (Sap =supu) ya mmea kwenye majani, matawi,mashina, maua hata mbegu hasa zikiwa changakama vitunda. Njia hii ndiyo pekee kwa waduduwa kundi hili kujipatia mlo ili waishi nakuzaliana. Katika kundi la pili kuna waduduwenye tabia ya kukata mashina na kuangushamimea michanga na wengine hutafuna majanina maua. Zaidi ya uharibifu katika kula mimea,wadudu wengi ni hifadhi ya viini vya magonjwaya virusi.

 2.Kundi la pili ni la wadudu waharibifu baada
ya mavuno kuwekwa ghalani.
 Athari ya wadudu hawa inapelekea wakulima kupoteza chakulaghalani pia kupunguza chakula ghalani piakupunguza ubora wa mazao yanapopelekwasokoni mfano Mahindi yanapofunguliwa sokolake ni duni. Jamii za wadudu na athari zaozinaelezwa katika aya zifuatazo:-
1. KUNDE:(ii) Foliage beetle (Ootherca mutabilis)Wadudu hawa hushambulia mimea ya kundebaada ya mbegu kuota (Seedling stage). Wakiwakwenye hatua ya mdudu kamili (adult stage)hushambulia majani kwa kula sehemu kati yavihimili vya majani (area between leaf veins).Mashambulizi ya wadudu wengi husababishammea kupoteza majani yote na hatimaye mmeakufa.Kuzuia jamii ya wadudu hawa:Dawa za chemikali aina ya endosulfan, Karaten.k. huagamiza mashambulizi kwa mpulizommoja.(i) Aphids (Aphis gaccivora)Hawa ni kati ya wadudu wenye kusababishahasara kubwa katika zao la kunde.Wanapendelea kula mvunga wa majani (underleaf), sehemu za vishina na hata vitumba (pools)vya mbegu. Athari za mashambulizi: Mmeahudumaa, majani husinyaa na kukunjamana piahupukutika kabla hayajazeeka hatimaye mmeahufa.Kuzuia Aphids: Dawa za kemikali aina yaphosphomiolon na dimethoate kwa cc 40 katikalita 10 za maji.(ii) Flower thrips (Megalurothrips sjostedti)Hatua ya mdudu kamili hushambulia maua.Mimea ikishambuliwa sana haizai matundakwasababu maua yameharibika. Mashambuliziyakiwa makubwa zao lote huangamia.Kuzuia: Kwa kutumia chemikali aina yaCypermethrin – kiwango cha cc 40 katika lita 10za maji.(iii) Podborers (Maruca testulalis)Wadudu hawa hula mvungu wa majani, ganda lashina na vitumba vya mbegu katika hatua yakukomaa. Athari: Mmea hudumaa, umbo lamajani huharibika (olistorted leaves) nahupukutika kabla ya kuzeeka. Mimea mingi hasamichanga hufa.Uzuiaji: Kwa kutumia chemikali aina yaphosphomidon na dimethoate kwa kiwango chacc 40 katika lita 10 za maji.(iv) Podsucking bugs (Anoplemenia,dentires,Acanthomia SPP)Wadudu hawa hushambulia mikunde katikahatua ya kuweka vitumba (pods). Hasara,inayosababishwa, na wadudu hawa hufikia 90%.Madhara makubwa huletwa na hatua ya wadudukamili (adult stage/ kwa kufyonza “Sap = Supu”ya vitumba teketeke ambavyo husinyaa nakukauka bila kukomaa wala kuwa na mbegu.Kuzuia: Kwa kutumia chemikali za Endosulfan audimethoate kwa kiwango cha cc 40 katika lita 10za maji.(v) Cowpea storage weevils (Callosobrunchusmacuhates callosobrun ams chinensis).www.kilimofaida.blogspot.comMashambulizi ya wadudu hawa wawili huanziashambani wakati kunde zimekaribia kukomaa.Wadudu hutaga mayai kwenye vitumbavilivyokomaa. Mayai yakiangauliwa, funzahupenya kupitia kwenye matoboyanayosababishwa na wadudu wengine. Funzawakianguliwa hushambulia mbegu na uharibifuhufikia 70% ya mbegu safi.Kuzuia: Tumia chemikali aina ya Acteric SuperDust 100 mg za unga wa dawa katika 10 Kg zambegu safi (Seed grain)
NAMNA YA KUZUIA MAGONJWA YA ZAO LA

KUNDE:Magonjwa hatari yanasababishwa na vimeleavya virusi na vya bacteria aina tabia na uzuiajiwa magonjwa haya ni kama ifuatavyo:-
(i) Cowper aphid-born mosaic virusUgonjwa huu husababishwa na virusi nahupelekea mkulima kupata hasara ya 13 – 87%ya zao.Dalili za ugonjwa huu ni michirizi yarangi ya kijani iliyochanganyika na njano au yaugoro (mosaic & mottling) kwenye majani.Kuzuia: Kwa kutumia aina za kunde zenyekustamili ugonjwa huu kama Tumaini, Fahari naVuli.
(ii) Bacterial blight (Xanthomonus vignicola)Ugonjwa huu hushambulia sana miche na kiasicha 60% ya miche yote hufa.Dalili: Majani,vitumba au mashina ya mimeailiyoathirika huwa na vidonda vyenye rangi katiya njano ya chungwa. Katika mashambulizimakubwa vidonda vidogo huungana (merge –coleasce) na eneo kubwa la majani huharibika.Ugonjwa hushamiri katika kipindi cha mvuanyingi (Kifuku) na umwagiliaji kwa juu (Overheadirrigation).Kuzuia: Tumia mbegu zinazovumilia ugonjwakama Tumaini, Fahari na Vuli.
(iii) Bacterial blight (Xanthomonas Spp)Ugonjwa hushambulia aina ya kunde pori nazinazolimwa.Dalili: Vidonda vidogo huonekana uvunguni mwamajani. Katika mimea dhaifu (more susceptible)vidonda huungana na kuwa na umbo la duaralenye ukubwa wa: kipenyo cha 1-3 cm.Mwanzoni vidonda huonekana kufutukamvunguni mwa jani kadiri vinapokomaa huwana rangi ya kahawia upande wa juu na majani.Baada ya muda vidonda hukauka na hubakishamigonyeo sehemu zilizoathirika. Majani mengiyaliyathirika hubadilika kuwa njano na baadayehuanguka / hupukutika.Ueneaji: Ugonjwa huenea kwa kasi wakati wakifuku (mvua nyingi) na umwagiliaji unapokuwawa juu. (overhead irrigation). Kimelea chabacteria huyu hudumu kwenye punje (mbegu).Kwa hiyo mbegu za namna hii huota zikiwa naviini vya ugonjwa.Kuzuia: Kutumia mbegu zenye kustahimiliugonjwa huu kama Tumaini, Fahari na Vuli

(iv)Powdery Mildew (Ukungu)
Dalili-Majani yanakuwa na vidoti vya njanoambavyo vinabadilika kuwa vya kahawia aukijivu haraka na ambapo kunakuwa na ungaunga katika majani.Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimiliukungu,Pulizia dawa za ukungu (Fungicide).anza kupuliza wiki tatu baada ya mimea kuotana kuendelea kulingana na hali halisi yaugonjwa.
UVUNAJI

Vuna kunde zako baada ya kukomaa na kuanzakukauka kwa kung’oa mashina au kuchuma kwamikono.Kisha zisambaze kunde zako aumashina yako juani ili zikauke zaidi na uwezekuziondoa kwa urahisi kutoka katika magandayake.

Unaweza kuondoa maganda yake kwamkono au kuupigapiga taratibu au kwakutwanga katika kinu taratibu bila kuzipasua.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 
Walter Emmanuel 0718 405318

Na Octavian Lasway Irrigation and water Engineer

+255763347985/673000103

Share:

Previous Post
UUZALISHAJI WA
Next Post
MATUMIZI BORA

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 1
  • IRRIGATION 5
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited