• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

MASWALI NA MAJIBU, TUNAWAJALI WAKULIMA WETU

Home / AGRONOMY / MASWALI NA MAJIBU, TUNAWAJALI WAKULIMA WETU
  • July 22, 2022

MASWALI NA MAJIBU

Moja kwa moja katika kuboresha kilimo tunawaletea maswali na majibu kama mlivyo uliza kwenye mitandao ya kijamii na magazeti 

Wataalamu ABDUL MKONO (MWL ABUU)  BSc AEA, SUA                      

Email : a2mkno@gmail.com Phone

0767359818 0652359818

ENGINEER  OCTAVIAN J LASWAY

BSc. IRRIGATION AND WATER RESOURCES ENGINEERING SUA

0763347985/0673000103

1. Kwa majina naitwa FRANK MSHANA natokea DODOMA nalima nyanya katika green house. Kuna ugonjwa unanisumbua sana Mtaalam kama unavyoona hapo katika picha. Je dawa yake ni ipi?

JIBU;Ugonjwa huo husababishwa na virusi viitwavyo kwa jina la kitaalamu Tomato leaf curl virus. Virusi husambazwa kutoka mimea iliyoathirika na kwenda kwenye mimea yenye afya kupitia kufyonza kwa nzi weupe (whiteflies), (thrips) na wadudu mafuta ambao kitaalamu huitwa  (aphids). Hivyo hakuna kinga maalumu ya virusi huyu ispokuwa kuzuia mashambulizi ya ugonjwa huu kuendelea kuenea maana huenea haraka sana. Kuzuia kuenea haraka tafuta dawa ya kupambana na inzi weupe, wadudu mafuta au thrips dawa hizo zipo nyingi hapa ntataja chache mfano  DYNAMEC, ACTARA na nyinginezo mojawapo ya hizo.Kwa faida ya wasomaji ugonjwa huu ni hatari sana hivyo bora mkajua dalili ya ugonjwa huu ili kuweza kukinga mara baada ya kuziona.

DALILI

Dalili zinajumuisha mmea kuwa na rangi ya manjano, mabaka, rangi za kahawia, kudumaa, kukunjika kwa majani, nafasi fupi baina ya vifundo, majani membamba. Mazao duni, kuchelewa kuiva kwa matunda, rangi isiyo sawasawa ya matunda ni matokeo ya mashambulizi. Lakini pia dalili za ugonjwa hutegemeana sana umri wa mmea ulioshambuliwa, hali ya mazingira, aina au jamii ya virusi vilivyopo lakini pia aina ya nyanya pia.Lakini pia mkulima ni bora afuate mbinu zifuatazo mapema kabisa ili aweze kujikinga na ugonjwa huu kwa sababu pindi uingiapo shambani hupunguza uzalishaji.

MBINU BORA ZA KILIMO

v  Fuata ratiba maalumu za upigaji wa dawa katika vipindi tofauti tofauti vya ukuaji wa mmea ili kukinga magonjwa hatarishi kwa mmea. Kitu ambacho wakulima wengi hawana ratiba hizo na wala hawazijui.v  Panda nyanya zilizokingwa na epuka mbegu za asili hasa za kukamua.v  Tumia chandarua au neti maalumu katika kuhifadhi miche isigusane na wadudu.v  Epukana na ardhi iliyolimwa nyanya kwa muda mrefu na zenye mimea iliyoathirika.v  Ng’oa mimea iliyoathirika na choma moto mabaki ya mazao.v  Fanya mzunguko wa mazao na mimea yenye kustahimili.v  Epuka kuvuta sigara wakati wa kuhudumia nyanya.v  Safisha mikono na zana kwa kutumia dawa za kuua vimelea vya magonjwa na epuka kwenda kwenye mashamba safi baada ya kutoka kwenye mashamba yaliyoathirika.

KUMBUKA

Mkulima unapaswa kujua ratiba maalumu ya upigaji dawa na sio kukurupuka mara baada ya kuona ugonjwa umeingia shambani. Wakulima wengi hukurupuka na kusahau kuwa ugonjwa huu ukishauingilia mmea hamna namna ya kuuokoa zaidi ya kuuondoa na kuuchoma. Na hapa mkulima anakuwa anaingia katika hasara maana hata idadi ya matunda yanayotegemewa kuvunwa hupungua.

2. jina langu naitwa DEOGRATIUS MAKISHE nipo Arusha, swali langu kuhusiana na mada iliyopita ya mbolea ya maji. Je mbolea ya maji inaweza kudumu kwa muda gani na njia gani sahihi ya kuhifadhi mbolea hiyo bila kuharibika?

MAJIBU: Mbolea ya maji huweza kudumu kwa muda wa siku saba tu na hapo huwa imeshaoza vyema na tayari kwa matumizi. Na ndio maana ili mkulima aweze kuweka mbolea kwa siku saba mfululizo anapaswa kuwa na madumu saba ili kila moja likikamilisha siku linatumika na kisha kuandaliwa upya. Ni vyema ikae siku saba kwani mbolea itakapolowekwa zaidi ya siku saba kuna uwezekano ikaleta wadudu waharibifu.Kuhusiana na kipengele kinachosema kuwa njia sahihi ya kuhifadhi. Kikubwa inapaswa kufunikwa ikiwa inaandaliwa na inapokamilisha siku saba yapaswa kutumika mara moja. Haitofaa useme utatazalisha mbolea nyingi sana ili upumzike na kuanza kuitumia labda kwa mwezi hivi. Jibu ni hapana kila wiki unapaswa kuandaa mbolea hii ambayo itakuwa ikitumika kila siku.
Usikose kusoma gazeti la mwananchi kila jumamosi ukurasa wa 33 ili ukutane na makala nzuri zenye kusheheni ujuzi na utaalamu wa kilimo 
bonyeza hapa kusoma makala nyingine kama drip irrigation system, Umuhimu wa kupima udongo

Share:

Previous Post
DRIP IRRIGATION
Next Post
MASWALI NA

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 1
  • IRRIGATION 5
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited