• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

NJIA NZURI ZA KUONDOA MAGADI(SALTS) SHAMBANI

Home / AGRONOMY / NJIA NZURI ZA KUONDOA MAGADI(SALTS) SHAMBANI
  • July 20, 2022

UtanguliziKatika mashamba mengi tatizo la udongo na ardhi kwa ujumla kujaa chumvi au magadi limekuwa tatizo kubwa kwa wakulima wengi kwani magadi au chumvi huleta madhara makubwa sana kwa mazao na hata mazao mengine hufa kabisa pale


yanapooteshwa kwenye udongo wenye magadi mfano wa mashamba yalioadhirika ni Ndungu irrigation scheme,kitivo irrigation scheme, Dakawa,Kiroka na Mkindo irrigation scheme (Morogoro), Kinyasugwe scheme (Dodoma) pia baadhi ya maeneo ya Lower moshi,Mawala,Kikavu chini, na hivyo kufanya mashamba yalio na tatizo hilo yasitumike katika uzalishaji,makala hii itakusaidia kujua namna ya kurudisha ardhi ya shamba lako katika hali nzuri na kuzuia uwezekano wa magadi kuongezeka katika shamba lako na hii itaongeza uzalishaji kwani utaweza kuotesha mazao mengi na ya aina mbalimbali kama udongo wako utakuwa na hali nzuri ya kuupatia mmea wako maji na madini or (nutrients) za kuuwezesha kukua vizuri na kuzaa sana

AINA ZA MAGADI ZILIZOPO KWENYE UDONGO 

Kuna aina nyingi za chumvichumvi zilizopo ardhini na huwa katika viwango tofauti kulingana eneo moja na lingine na tofauti hii husababishwa na asili ya udongo wa mahali husika chumvi hizi ni kama Sodium ambayo hupatikana kwenye chumvi ya kawaida(NaCl), Potasium, Boron,Magnesium, Calcium, Phosphorous madini mengine ni muhimu katika ukuaji wa mmea lakini kwa kiwango kinachotakiwa na huwa ni sumu endapo yatazidi kiwango chake

NAMNA AMBAVYO MAGADI HUDHOOFISHA MIMEA

Madhara yatokanayo ma magadi ni makubwa sana na huleta hasara kwa wakulima wengi sana, kitaalamu magadi huzuia mizizi ya mimea kufyonza maji kwenye udongo na kuufanya mmea kushindwa kukua kwani maji ni muhimu katika mfumo wa mimea kujitengenezea chakula chake hata kama utamwagilia maji ya kutosha katika shamba lenye magadi bado mimea haitaweza kupata maji hayo (salts induce water stress to crops through matrix forces build up between the soil particles and the salts ion and hinder plant water uptake via capillarity and osmosis). Pia magadi huharibu mfumo wa udongo(soil structure) na kuufanya udongo kuwa mgumu na kuzuia mizizi ya mmea kupenya vizuri kwenye ardhi na hivyo kupunguza udhabiti wa mimea iwapo shambani na kusababisha kuanguka angauka kwa mazao yanapofikia wakati wa kubeba matunda au maua kwani hukosa nguvu za kujishikilia kwenye ardhi na hali hii husababishwa sana uwepo na sodium nyingi shambani na mkulima hupata hasara kubwa sana.

VYANZO VYA MAGADI KWENYE UDONGO

  • Asili ya udongo wenyewe 

Baadhi ya maeneo yana udongo wenye asili ya chumvi kwa Tanzania maeneo hayo yanapatikana kwa wingi dodoma na singida na hasa wakati wa kiangazi baada ya mvua kukatika unaweza ukaona kabsa mabonge ya chumvi ardhini

  • Maji yanatumika kwa umwagiliaji 

Kuna baadhi ya maeneo maji yake huwa na chumvi kiasi  kwenye mito na hapa chemichemi na wakulima hutumia maji kutoka kwenye vyanzo hivyo vyenye maji ya chumvi katika kumwagilia mashammba yao, hii huongeza chumvi kidogo kidogo kwenye ardhi na kama mwendelezo wa kutumia maji hayo utafanyika kwa miaka mitano basi shamba hilo litakuwa limejaa chumvi na halitafaa tena kwa kilimo endapo njia na mbinu stahiki hazitachukuliwa

  • Utumiaji wa mbolea za viwandani bila maelekezo ya kitaalamu

Tujue ya kuwa sio kila mbolea ya kiwandani inafaa kwenye kila aina ya udongo, pili tunapokuwa tunaweka mbolea shambani lazima tuwatumie wataalamu ili watupe vipimo sahihi vya uwekaji wa mbolea hizi ili ziwe kwa kiwango kinachotakiwa pasipo kuzidisha wala kupunguza , kila shamba lina rutuba tofauti na lingine kwa hiyo ata uwekaji wa mbolea utatofautiana, pia kila zao lila vipimo vyake vya kiasi cha mbolea kinachotakiwa, kumbuka ni muhimu kufuata ushauri wa wataalamu kabla ya kuweka mbolea shambani ili kuondokana na matatizo na uweze kuzalisha mazao yenye tija ndio maana wataalamu kutoka Green Agriculture tunakushauri upime udongo kwanza kabla hujaanza kulima

  • Mfumo mbaya wa utoaji maji shambani(poor drainage system)

Tatizo hili ni kubwa sana hasa pale wakulima wengi wanapoamini kuwa katika kumwagilia shamba lazima aone maji yametuama ndio aridhike kuwa amemwagilia, hili ni kosa kubwa kwani tunatakiwa tujue kuwa mimea hufyonza maji yaliyo ardhini tuu(plants absorb water, and they don’t drink water ……… Myth), maji yaliyotuama shambani hupandisha chumvi iliyopo chini kuja juu na baada ya ardhi kukauka chumvi ile hubakia juu ya ardhi na kuathiri mimea

NJIA ZA KUONDOA MAGADI SHAMBANI

Hili ndilo lengo kuu la makala hii ili kumsaidia mkulima kuondokana na tatizo hili, nitaeleza njia za kitaalumu na za gharama nafuu za kuondoa na kupunguza magadi shambani.

  1. Kuzamisha chumvi(Leaching of salts)

Wakati wa kumwagilia shamba unashauriwa umwagilie maji mengi kiasi kuliko yale yanayotosheleza mmea wako ili maji hayo ya ziada yasaidia katika kuzamisha chumvi iliyoko juu wa udongo iende chini zaidi ambako mizizi ya mimea haifiki, njia hii lazima utumie wataalamu wa umwagiliaji (irrigation engineers) kama mimi ambao tutakusaidia kitaalamu kuendena na udongo wako na tutakuambia ni kiasi gani cha maji inatakiwa umwagilie katika shamba lako ili kuondoa chumvi na kusaidia mimea yako kukua (irrigation and leaching requirements)
     2. Uwekaji wa Gypsum (Calcium Sulfate)Gypsum hufanya kitu kinachoitwa neutralization ambapo hubadilisha chumvi iliyopo ardhini isilete madhara kwa mimea na katika maduka mengi ya pembejeo zinauzwa hizi gypsum kwa ajili ya mashamba ili kudhibiti chumvi na magadi lakini njia hii ni ya gharama kidogo     3. Utumiaji wa Samadi Mbolea za wanyama na mimea husaidia sana kwenye kuongeza rutuba kwenye ardhi pia katika kuhakikisha na kupungiuza magadi kwenye udongo na njia hii matokeo yake ni polepole lakini ina uhakika na pia samadi ina faida nyingine nyingi katika kuimarisha udongo na kuongeza upatikanaji wa madini kwa mimea
   4. Njia ya mafuriko (flooding)Njia hii hufanywa katika maeneo yenye maji mengi na hasa kipindicha mvua , shamba lenye magadi hutifuliwa na kufurishwa au kumwagiliwa mpka maji yanatuama (wakati hamna mazao shambani) na baada ya hapo maji hutolewa kwa mifereji maalumu na maji hayo huchukua magadi katika shamba husikaNB. njia hii usiifanye kwenye mashamba yaliosongamana ili maji yaliyo na magadi yasiende kwenye shamba la jirani yako na kumpa hasara        5. Utumiaji wa njia za kisasa za kufanya umwagiliaji kama drip irrigation,sprinkler system hupunguza uwepo wa magadi kwenye udongo na kama unahitaji system hizi nitafute kwa mawasiliano mwishoni mwa makala hiiLakini kwa maeneo ambayo yana magadi sana unashauriwa kupanda mazao yanayoshahimili ardhi yenye chumvi mazao yanayoshahimili chumvi zabibu,mbaazi,Nanasi,Miembe hasa mazao ya miti ndio hushauriwa sana katika ardhi yenye magadi mazao yasiostahimili udongo wenye magadi Mahindi,Tikiti maji,Nyanya, Mbogamboga, na mengne mengi fuata ushairi wa kitaalamu kabla ya kuanza kulima na kupanda Kwa ajili ya kupima udongo na ushauri wasiliana na mimi mwenyewe kwa number za simu hapo chini
SOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA KILIMO HAPAbofya hapa chini

Kilimo bora cha tikiti maji, kuhusu bustani za mboga, mbinu bora za kulima vitunguu 

Eng Octavian Justine Lasway 

Bsc irrigation and water Resources Engineering  

Sokoine University of Agriculture(SUA) 

Phone. 0763347985/0673000103   

Email . lasway@greenagriculturetz.com                   

Share:

Previous Post
FAHAMU NAMNA
Next Post
PATA MATOKEO

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 1
  • IRRIGATION 5
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited