• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

UZALISHAJI WA TIKITIMAJI

Home / AGRONOMY / UZALISHAJI WA TIKITIMAJI
  • July 20, 2022

Tikitimaji ni zao la kitropiki linalo tumia siku 65-90 kutoka kupandwa hadi kuvunwa kulingana na aina ya mbegu uliyotumia na hali ya hewa ya eneo husika kwani maeneo ya pwani na yenye joto sana tikitimaji na mazao mengine hukomaa mapema ukilinganisha na maeneo ya milimani yenye baridi kwa hiyo tunashauri kama unataka kulima tikitimaji basi tafuta sehemu zenye hali ya hewa nzuri kuendana na mahitaji yako na soko lako lilivyo

ENEO

Chagua eneo ambalo halina historia ya kuwa na magonjwa au wadudu wanaoshambulia tikiti maji.Eneo ambalo maji yanapatikana kwa urahisi kwa ajili ya umwagiliaji wa tikiti maji ,pia eneo lisilo na udongo wenye chumvi chumvi na unaotuamisha maji soma hapa kujua aina za udongo Namna ya kutambua udongo wenye chumvi na namna ya kuondoa chumvi,Njia za kupima na kutambua aina ya udongo kwenye shamba lako, tikiti maji linastawi sana katika udongo tifutifu na kichanga lakini udongo wa mfinyanzi sio mzuri sana kwa tikiti maji kwani husababisha matunda kuwa na nyufa(cracks)

KUANDA SHAMBA.

Lima shamba lako vizuri kwa kuvunja vunja udongo na pia andaa matuta yenye upana wa mita 2 na urefu kwenda juu sentimita 30 ili kusaidia mizizi ya tikiti kukua vizuri na kuzuia maji kutuaama hasa katika kipindi cha mvua.mfano wa picha kwa uandaaji wa shamba.

MFANO WA MASHAMBA YALIYOLIMWA VIZURI TAYARI KWA KUPANDA

Nikaribishe kwenye shamba lako nikupe utaalamu namna ya kuandaa shamba kwa ajili ya kilimo hiki na mazao mengine
MAHITAJI YA TIKITIMAJI
Tikiti linakua vizuri katika udongo unaoshika maji vizuri lakini yasio tuama na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji.Udongo wenye pH 5.8-6.6.pia kama pH ni ndogo tutakushauri cha kufanya ili iweze kuwa nzuri na ya kiasi kwa ajili tikitimaji. 
Tikiti halistawi vyema ktk baridi na linahitaji joto la udongo kiasi cha 18-29 0c. 
Joto chini ya 18 0c na juu 29 0c litaathiri kuota kwa mbegu na ukuaji wa mmea.Katika kipindi cha ukuwaji tikitimaji linahitaji unyenyevu wa udongo wakati wote lakini maji yakizidi katika udongo wakati wowote wa ukuwaji na uwekaji wa matunda hupelekea upasukaji wa matunda na kupunguza mavuno na ubora wa matunda.


UPANDAJI
Mbegu/mche wa tikiti maji utapandwa mita 1-2 kati ya mmea na mmea na uwekwa sentimita 2.5 kwenda chini(shimo la kupandia), na kati ya mstari na mstari iwe mita 2,kwa umbali huu panda mbegu 2 kila shimo.Au weka umbali wa sentimita 50 kwa mita 2 lakini hapa panda mbegu moja moja. katika hekari moja utahitaji mbegu gramu 500gms-600gms.


UTUNZAJI WA MMEA.
a) Mbolea.
Mbolea ya samadi kwa kiasi cha 4-6 tani kwa ekari,ichanganye na udongo wiki moja kabla ya kupanda,pia mbolea hii unaweza iweka katika kila shimo siku kadhaa kabla ya kupanda kisha mwagilia ili kupunguza kiasi kikubwa kitakacho hitajika kuweka katika ekari moja.Kama huna samadi tumia Yaramila winner au DAP weka gram 5 kwa kwa kila shimo ,hakikisha mbolea na mbegu havigusani.


Wiki mbili baada ya miche yako kutokeza weka mbolea ya kiwandani -N-P-K (Yaramila winner) gram 5 tena kwa kila shimo,hakikisha unaichimbia chini na isigusane na mmea.


Weka mbolea yenye Calcium kana Yaramila nitrabo gram 10 kwa kila shina unapoona matunda yameanza ili kusaidia kupata matunda makubwa na mazuri.


UMWAGILIAJI
Maji kwa sentimita 1-5 katika udongo yanatakiwa kwa mvua au umwagiliaji ili kupata tikitimaji zuri,kipindi cha muhimu sana kwa mahitaji ya maji kwa tikitimaji ni :kabla ya mche kutokeza ,mwanzo wa kutoa maua na siku 10 za mwisho kabla ya kuvuna.Maji machache kipindi cha kupanda husababisha kutoota kwa mbegu,kipindi  cha kuweka maua husababisha matunda machache kutokeza na matunda kukosa maumbo yake.Siku 10 za kuelekea kuvuna husababisha matunda kuwa madogo kama maji ya kutosha yasipopatikana.Matunda yakielekea kuiva punguza umwagiliaji maana kiasi kikubwa cha maji kitasababisha kiasi kidogo cha sukari kutengenezwa na kupasuka kwa matunda, pia kumbuka kweka mfumo wa utoaji maji shambani yaani drainage sytem(nitakuonyesha zaidi nikifika shambani kwako) hii itasaidia kuondoa chumvi na kuhakikisha mazao yanastawi vizuri


Angalizo:
Usimwagilie jion sana hii itasababisha kukua kwa magonjwa kwa sababu ya kuacha majani ya mmea yakiwa na unyevunyevu .Pia angalia wakati mzuri wa uchavushaji /wakati ambao  nyuki wanakuwepo shambani mwako hivyo jitahidi kumwagilia mda ambao hautawasumbua nyuki.


Matandazo.
Ni muhimu kutumia matandazo katika shamba lako ili kusaidia kutunza unyevunyevu katika udongo na matandazo haya baadaye yakioza uongeza rutuba katika udongo na pia kusaidia kuzuia kumea kwa magugu na husaidia tunda kutogusana na udongo kitu ambacho kinaweza kusababisha tunda kuathiriwa na joto la udongo au magonjwa kirahisi.Weka matandazo pale mche wako utakapo fikia urefu wa sentimita 10.


Punguza urefu wa mmea
Ili kupata matunda mazuri na yenye afya ni vema kuupunguza mmea kwa mbele ,pale unapoona mmea umefika urefu wa kutosha ili kusaidia kutengeneza matawi ya pembeni ambayo mara nyingi ndio ubeba maua ya kike.

Kuondoa magugu


Ni muhimu sana kuondoa magugu katika shamba lako hasa wiki za mwanzo ili kuzuia ushindani  wa mahitaji kati ya magugu na mmea ambapo hupelekea kupungua kwa mavuno na muda mwingine magugu haya yanaweza kuwa ndio chanzo cha baadhi ya magonjwa katika mmea wako


Uchavushaji
Ili kupata kiasi kikubwa cha matunda ni vyema kuwa na mzinga wa nyuki karibu na shamba lako ili kusaidia uchavushaji wa maua ya tikitimaji.Tunashauri uwe na mizinga 1-2 kwa hekari moja.Waweza pia pands alizeti jirani na shamba lako ili kuvuta nyuki.Pia zuia kupulizia dawa za wadudu kipindi cha maua maana unaweza wakimbiza au kuwaua nyuki, kumbuka maua ambayo hayakuchavushwa vizuri huzaa matunda yenye umbo baya lisilo shabihiana na mengine.

Punguza idadi ya matunda
Kwa kawaida tikitimaji uweka zaidi ya matunda manne ,ili kupata matunda makubwa na yenye afya ni vyema kupunguza matunda kwa kuondoa baadhi ya matunda ambayo yanaonekana hayana afya nzuri na yaliopoteza umbo zuri na kuhakikisha kila mche unabaki na matunda 2-3 tu.


Uvunaji
Tikitimaji uvunwa baada ya miezi miwili na nusu hadi mitatu kutoka siku ya kupanda,lakin yapo ambayo hukomaa kwa siku 60-75 kutokana na aina ya mbegu.
 Mangonjwa
 
1) Ubwiru chini (Downy mildew)
Huu ungonjwa husababishwa na fangasi (Pseudoperonosporacubensis).Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani na hupendelea sana wakati wa baridi,
 Dalili zake:
Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka  na madoadoa meus kwa mbali..


Tiba yake.
Tafuta dawa yenye viambato…Metalaxyl na mancozeb ….kama vile Ridomil gold.


2) Ubwiru juu (Powdery mildew ) 
Dalili za huu ungonjwa…utaona majani yanakuwa kama yamemwagiwa unga ua majivu


Tiba yake
Tafuta dawa yenye kiambato…Difenoconazole ..kama vile Score.


3) Kata kiuno.(Damping off)


Huu ugonjwa husumbua sana miche midogo,huanzia aridhini ,husababisha miche midogo kuanguka chini baada ya kula sehemu ya shina.


Tiba yake.
Tafuta Ridomil gold na anza kupulizia mara tu baada ya mimea yako kuota.
 Wadudu
1) Wadudu mafuta (Aphid)
Hawa hushambulia majani na kufyonza juis ya mmea na baada ya kushambulia majani hujikunja na baadaye kupelekea mangonjwa ya virusi.


Dawa yao.
Tafuta Actara na pulizia majani pamoja na udongo.


Wadudu wengine ni;Nzi weupe (whitefly )-Actara itawamaliza.


,Utitiri mwekundu (Redspidermites)-Dynamec itawamaliza,Thrips-Actara na Dynamec itawamaliza kabisa.



Mbegu bora za tikitimaji.
Kuna mbegu chotara na opv(Sio chotara)
But mbegu bora ni chotara na baadhi ya hizo mbegu ni…


1) Sukari F1-Kutoka East Africa seeds.
2) Sugar king F1-kutoka africasia
3) Juliana F1-kutoka Kiboseed
4) zebra F1-Kutoka Balton.


ambazo zinapatikaana dukani kwetu kwa bei nafuu na ni mbegu bora 

SOKO LA TIKITI 
Napenda kuwashauri wakulima wetu kuwa njia nzuri ya kulima tikitimaji ni ile ya umwagiliaji, ukiwa mkulima wa tikitimaji lazima uwe mjanja kupanda zao lako ili uje uvune wakati soko liliwa vizuri, mzunguko mzuri wa kupanda tikiti ni huu, panda zao lako katikati ya msimu wa mvua wakati walimaji wa matikiti kwa kutegemea mvua (ambao ni wengi) mazao yao yametoa maua ili wakati wao wanavuna tikiti zao, mazao yako yawe ndio yanaanza kutoa maua kwa hiyo wakati unavuna wakulima wa kutemea mvua watakuwa washamaliza soko lao.Pia kwa wale wanaotegemea mvua ni vizuri uchunguze soko lako vizuri ili uwe na uhakika wa kuuza matunda yako wakati yakiwa tayari yamekomaa.



ukihitaji makala hii kwa mfumo wa Pdf nipigie kwenye number za simu hapo chini



Agronomist Boniphace Mwanje
0719880905
&
Engineer Octavian Lasway 
Irrigation and Water resources Engineer

Share:

Previous Post
MWONGOZOWA KILIMO
Next Post
FAHAMU NAMNA

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 5
  • IRRIGATION 1
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited