KILIMO BORA CHA MIEMBE , UCHAGUZI WA MBEGU , UPANDAJI , UTUNZAJI NA MASOKO

Embe ni tunda linalotokana na mti wa muembe, hupandwa kwa njia ya mbegu  kutoka kwenye tunda lilokwisha komaa au kuiva vizuri.

NAMNA YA KUANDAA MBEGUMbegu nzuri huchaguliwa kutoka kwenye tunda lenyewe na kumenywa vizuri kwa ajili ya kuchukua kiini cha ndani, baada ya kutoa kokwa la nje, baaada ya hapo mbegu hufungwa vizuri kwenye tissue na kuachwa siku tatu (3) ikiwa ndani ya mfuko wenye unyevu kiasi, na siku ya 3 hutolewa na kupandwa kwenye kiriba, pia unaweza kuipanda moja kwa moja kwenye kiriba bila kuifunga kwenye tissue, faida za kuifunga kwenye tissue ni kuirahisisha kuota mapema.

NAMNA YA UPANDAJI WA MBEGU KWENYE VIRIBA.kwanza viriba huandaliwa kwa kujazwa udongo mzuri wenye virutubisho vya kutosha, na upandaji wa mbegu hufuata, weka shimo kidogo ndani ya kiriba chako na weka mbegu kwenye hilo shimo,upande wa mgongo (chini) wa mbegu yako uwe juu na upande wa kiini uwe chini, baada ya hapo rudishia udongo wako taratibu na mwagilia maji kiasi.Pia wengine hupanda mbegu moja kwa moja shambani bila kukuzia kwanza miche kwenye kitalu. baada ya hapo miche huachwa na kukua baada ya miezi 3 huhamishiwa shambani.
Katika uzalishaji wa zao la miembe kuna njia mbili,  kuna ambayo; 1.huchukua muda mrefu  kukua  2. huchukua muda mfupi kukua hadi kufikia tunda     (miche ya kisasa) 
Inayochukua muda mrefu kukua ni ile ambayo hupandwa moja kwa moja shambani na kuendelea kutunzwa hadi kufikia tunda, huchukua miaka 7 hadi 15, 
muda mfupi ni ile inayofanyiwa kiunganishi (grafting) kutoka kwenye mche wenyewe (root stock) na kikonyo (scion) kutoka kwenye mti mkubwa ambayo tayari ulishatoa matunda, Miche ya muda mfupi huchukua miaka 2.5 hadi 3 tayari kwa kuanza kutoa matunda.

FAIDA ZA KUUNGANISHA (GRAFTING) KWENYE MICHE YA EMBE.

  • hufanya mche uweze kukua kwa haraka na urahisi vizuri
  • hutoa nafasi ya kuchagua ni aina gani ya embe unahitaji kuzalisha kulingana na soko au upendeleo wako mwenyewe
  • huvumilia kushambuliwa na magonjwa na wadudu
  • unaweza kuzalisha maembe kipindi ambacho sio msimu wake.

aina za embe zinazotokana na kuunganisha au (grafting) ni Tommy, Kent, Red Indian, Alphonso,Keit, Dodo pamoja na bolbo buyuni, yote hupendelewa sana sokoni.

NAMNA YA UPANDAJI WA MICHE YA EMBE.
Kuchimba mashimo.Miche ya embe hupandwa kwa nafasi ya mt  7-7 kati ya mche na mche na mt 7-7 kati ya mstari na mstari shimo linatakiwa  liwe na kina cha ft-3 na upana kutegemea hali ya udongo. Wakati wa kuchimba shimo udongo wa juu (wenye rutuba) na ule wa chini (usio na rutuba) lazima utenganishwe wa juu unaweza kuwekwa kulia na  wachini kushoto .
Kufukia mashimo.Chukua samadi debe 1-2 changanya na udongo wa juu (ulioweka kulia) jaza mchanganyiko wa samadi na udongo ndani ya shimo hadi utengeneze mwinuko wa kitako cha 100 cm toka usawa wa ardhi,Kupanda miche.Kata mizizi inayotokeza nje ya mfuko, kabla ya kutoa, weka mche ndani ya shimo kisha chana hiyo nylon na kutoa taratibu hiyo nylon ili udongo usiachane na mizizi, ukishindilia kiasi, fukia shimo kwa udongo hadi kufikia sehemu inayotenganisha shina na mizizi ya mche. 

Namna ya kutunza miche baada ya kupanda.Magugu huzuia miche kukua vizuri wakati ikiwa midogo au michanga, wakati wa kupalilia hakikisha hauharibu mizizi kwa kuikata.
Kilimo mseto.Wakati miembe ikiwa michanga panda mazao ya muda mfupi katikati ya mstari kama vile kunde na maharage kwani mazao haya huzuia magugu kuota  na huongeza rutuba na thamani ya shamba.
Kuweka matandazo (mulching).Nyasi  (mulching) husaidia kuhifadhi maji ardhini na hupunguza uotaji wa magugu na pia ya kioza huongeza rutuba ya udongo, hakikisha shina haligusani na matandazo ili kupunguza athari za mchwa na moto.

NOTE:  Miche iliyo tayari ya miembe pamoja na miche mingine yote ya matunda kama vile parachichi, machungwa, chenza, ndimu, limau, passion, mapera,komamanga,papai fenes, stafeli miti ya mbao n.k inapatikana,

kwa huduma ya uzalishaji, utunzaji pamoja na ushauri wa miche mbalimbali ya matunda na upatikanaji wake tunapatikana Morogoro- Nanenane, popote ulipo pia tunakutumia.

Veronica J Joseph 
Bsc Horticulture
Phone; 0766856431
Email:veronicajj94@gmail.com