UFUGAJI WA SAMAKI KISASA NA KIBIASHARA

UTANGULIZI

Ufugaji samaki ni kazi ya kupanda, kukuza na kutunza samaki katika mabwawa, mito, mifereji au eneo lililotengwa kwa ajili ya ukusanyaji wa maji, uzio (uliotengenezwa kwa vyuma, nyavu 
au miti) au eneo lolote ambalo udhibiti wake uko chini ya mamlaka ya mfugaji mwenyewe. Mabwawa  ya samaki hutengenezwa au huchimbwa kwa njia tofauti tofauti, yaweza kuwa ni ya 
kuchimbwa na watu (japokuwa ya asili pia huweza kutumika) Samaki pia wanaweza kufugwa baharini au ziwani kwa kutumia vizimba (cages) Pia uzio unaweza kuwekwa katika eneo lolote lililo na maji kama ziwa au baharí au chemichemi.

SATO

Sato /Tilapia wapo wa aina tofauti tofauti kama vile sato wa Mosambique, sato weusi, sato wa victoria na wale shiranus. Tofauti zao ni ndogo sana na mara nyingi ni vigumu kuwatambua.Ufugaji samaki kwa kiasi fulani si sawa na ukuaji wa samaki katika mito, maziwa na bahari. Tofauti iko katika huduma inayotolewa kwa samaki wafugwao na idadi ya samaki wanaopaswa kuwamo ndani ya eneo husika. Samaki waliofugwa huhitaji kulishwa na kuhudumiwa.

SAMAKI AINA YA KAMBALE

 Kambale (Claries gariepinus), ni aina ya samaki ambao wanafugwa kwenye maji baridi na wanauwezo wa kustahimili mazingira magumu kulinganisha na samaki wengine.Samaki hawa wapo species au wanatajwa kwa majina mbalimbali kulingana na eneo na jamii husika. Samaki hawa unaweza kusikia wakitajwa kwa majina mengine kama vile, kambale channel, koleo, samaki kidevu, samaki wa kwenye matope. N.k. Samaki hawa (kambale) wanakua kwa kiasi kikubwa sana kwanzia kilo 1 na kuendelea. Kambale hawana magamba na wanauwezo wa kustahimili upungufu mkubwa wa oxygen kwenye maji ya bwawa kwakua na mifumo miwili ya upumuaji katika mwili wao.Ufugaji wa samaki ni sector inayokua kwa kiasi fulani licha ya changamoto zinazo ikabithi sector hii hapa Tanzania. Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakifuga samaki katika mabwawa hata kabla ya nchi yetu kupata uhuru. Lakini baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitoa matunzo hafifu kwa kutofahamu vizuri mambo ya kuzingatia katika swala zima la ufugaji wa samaki kiasi cha kufanya mavuno kutokua mazuri na kupelekea sector hii kushuka na kukua kwa kusua sua. Kwa miaka ya karibuni, serikali imetilia mkazo utoaji elimu (ugani) wa ufugaji samaki ili kuboresha mafanikio yake.Green Agriculture co.limited tumekuletea kitabu cha UFUGAJI WA SAMAKI KISASA NA KIBIASHARA, kilichojaa maarifa na utaalamu juu ya ufugaji wa samaki kwanzia mwanzo, namna ya kuandaa eneo la kufugia samaki, mbegu ya samaki, chakula cha samaki,  uzalishaji  wa samaki, (sato na kambale), magonjwa na viumbe waharibifu kwa samaki. Wasomaji wetu wa kitabu hiki watasaidika kuongeza uelewa zaidi kwenye ufugaji wa samaki hususani kwenye uzalishaji wa samaki kama ufugaji wenye tija kwa manufaa ya mkulima ama mfugaji.Kitabu chetu kinapatikana kwa njia ya Hard copy kikiwa na kurasa zake 49 kumrahisishia mkulima katika usomaji.

Kupata kitabu chetu wasiliana nasi kwa+255752799673 / 0655859810.Godfrey, Christopher Sway
 Mtaalamu wa Samaki kutoka
 Sokoine University of Agriculture
 +255752799673 / 0655859810
Kwa mahitaji ya ushauri, utengenezaji na utunzaji wa mabwawa ya samaki wasiliana nasi