• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO NYUMBANI KWAKO

Home / AGRONOMY / JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO NYUMBANI KWAKO
  • July 21, 2022

JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO NYUMBANI

Kuna njia mbali mbali waweza kuepuka kutumia mboga mboga zinazolimwa usikokujua na kuepuka kujiingiza katika afya mbaya kwa matumizi ya kemikali za kuulia wadudu na magonjwa zinazotumika katika ukuzaji wa mboga mboga.

Aina za bustani

1. Unaweza tumia makopo amabayo mara nyingi hutumika kupanda maua kando kando ya nyumba2. Unaweza tumia gunia la sandarusi kubwa..3. Unaweza tengeneza key hole garden ( bustani ya tundu la Ufunguo)

Bustani Ya Makopo/Ndoo 

VifaaUdongo, makopo/ndoo, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri.Udongo – Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmeaMchanga/Rice husk – Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa. Mbolea ya samadi – Kutoa virutubisho kwa mmeaHatua za utengenezaji.- Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.   5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga/rice husk- Toboa makopo yako kwa chini ili kuzuia maji kubaki kwa wingi kwenye kupo na weka pamba kwenye matundu uliotoboa.- Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye makapo/ndoo. Hapo utakuwa tayar kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote. – Kuepuka uchafuzi wa mazingira kwa maji yanayo toka kwenye makopo endapo makopo hayo yapo kwene simenti, weka makopo/ndoo hayo juu sahani/besenUangalizi.- Mwagilia mboga yako mara tu baada ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.- Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kemikali za viwandani kama vile  majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku.- Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.- unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii inategemeana ni aina gani ya mboga)Faidi- Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani- Gharama za uhitaji wa mboga za majani.SEHEMU YA PILI 

BUSTANI YA GUNIA

VifaaUdongo, Kokoto (mawe madogo madogo), Gunia, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri, mti/mbao na kopo dogo (sadolini).Udongo – Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmeaMchanga/Rice husk – Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa. Kokoto  – Kusadia maji kupita ndani ya gunia toka juu hadi chiniMbolea ya samadi – Kutoa virutubisho kwa mmeamti/Mbao  – Kusaidia gunia lako kusimama vyema/ imaraHatua za utengenezaji.  (i)   Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.         5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga/rice husk.(ii)    Toboa kopo lako na ondoa kitako ili kuweka uwazi pande zote mbili (juu na chini)(iii)  Weka mti/ubao katikati ya gunia ukiuchimbia ardhini kisha weka kopo lako katikati ya mti/mbao hiyo na lijaze kokoto (iv)  Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye gunia lako ukilizunguka kopo lenye kokoto hadi kufikia kimo cha kopo. Baada ya hapo ondoa kopo na hakikisha kokoto zinabaki zikizungukwa na udongo.(v)  Weka kopo juu ya kokoto zilizozungukwa na udongo kisha, lijaze kopo hilo na kokoto, rudia kujaza udongo ukilizunguka kopo hadi kimo cha kopo hilo. Endelea kufanya hivyo (kama hapo juu) hadi pale gunia lako litakapokuwa limejaa. (vi) Toboa gunia kwa kuweka matundu kuzunguka gunia kwa ajili ya kupandia katika umbali sawa (inategemea na aina ya mboga) (vii) Hapo utakuwa tayari kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote juu na pembeni ya gunia lakoMboga aina ya letuce (Lactuca sativa) Mboga aina ya sukumawiki (Brassica carinata) zikiwa zimepandwa kwenye guniaUangalizi.- Mwagilia mboga yako mara baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.- Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kikemikali za viwandani kama vile  majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku.- Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.- unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii inategemeana ni aina gani ya mboga)Muhimu: Ukitumia miche kwa siku tatu/mbili za mwanzo usije ogopa kuona miche yako imelala endelea kuimwagilia itasimama tu. Pia katika umwagiliaji hakikisha unamwaga maji katika kati ya guni pale kulipo na kokoto ili kuhakikisha maji yanasamba ndani ya gunia hadi chini.Faidi- Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani- Gharama za uhitaji wa mboga za majani.- inatumia nafasi ndogo na kutoa kiasi kikubwa cha  mboga mboga.

KWA WALE WANAOHITAJI MAFUNDISHO HAYO NYUMBANI KWAAJILI YA KILIMO HIKI WANITAFUTE KWA NAMBA HIZO CHINI NA NIJE NYUMBANI KWAKO KUKUFUNDISHA KIVITENDO.


pia soma zaidi kuhusu klimo cha tikiti maji,kilimo cha tangawizi,namna nzuri ya kulima vitunguu maji

Octavian Justine Lasway 

Irrigation and water resources Engineer 

Sokoine University of Agriculture 

Share:

Previous Post
HATARI VIWAVI
Next Post
MCHANGANUO WA

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 1
  • IRRIGATION 5
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited