• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

NAMNA  NZURI YA KUPIMA UDONGO.

Home / Uncategorized / NAMNA  NZURI YA KUPIMA UDONGO.
  • July 17, 2025

Ni muhimu sana kufahamu aina ya udongo kabla ya kuanza kilimo cha zao lolote hii itakusaidia kupata mazao bora Zaidi na kwa wingi iwapo pia utunzaji mzuri utazingatiwa.

              Maeneo mengi hapa nchini yana udongo tofauti tofauti kulingana na hali ya eneo hilo, kuna maeneo yenye udongo wa kichanga, mengine yana udongo wa tifutifu  na mengine yana udongo wa mfinyazi, 

     Udongo wa kichanga, huu hupitisha maji kwa haraka na mara nyingi hauna rutuba ya kutosha kwa mimea, hupendelewa kwa kilimo cha mazao machache ya mboga mboga iwapo pia utachanganywa na mbolea ya samadi ya kutosha,  

Mara nyingi maeneo ya namna hii huwekewa mbolea ya samadi kabla ya msimu wa kupanda kuanza. 

    Udongo wa tifutifu, huu ni udongo wenye rutuba, mazao mengi hustawi sana kutokana na kuwepo kwa virutubisho vya kutosha, mara nyingi wa kulima wengi hushauriwa kutafuta maeneo yenye udongo wa namna hii, humpatia mkulima faida kubwa bila gharama ya kutumia mbolea nyingi iwapo pia atazingatia huduma nzuri kwenye mazao yake.

     Udongo wa mfinyanzi, haupitishi maji kwa haraka na mara nyingi hutuamisha maji,  haufai kwa mazao mengi kwa sababu  hushikana sana ambapo husababisha kutoruhusu hewa na maji kupita kwenye mmea hivyo huzuia ukuaji wa mmea.

Ili mazao yako yawe na afya bora shambani lazima udongo wako upimwe na udongo mzuri uchaguliwe ili kuweza kufahamu ni virutubisho gani muhimu vinahitajika na kwa kiwango gani.

         Udongo lazima uwe na uwiano sahihi wa pH, pH ni kipimo cha alkaline na acid kwenye udongo, uwiano huu husaidia kujulisha kama udongo wako una virutubisho vyote au hauna,

Acid huanzia 0 hadi 6 na alkaline huanzia 8 hadi 14, na 7 ni neutral  (uwiano sahihi wa pH kwenye udongo)  na ndio unao faa kwa mazao mengi na mara nyingi hufanya vizuri zaidi.

Iwapo udongo wako utakuwa una tindikali ( acid) nyingi Zaidi unaweza kutumia chokaa (lime) ili kushusha kiwango cha tindikali na kuweka uwiano sahihi.

Namna ya kuongeza au kupandisha pH,  kiwango cha chokaa (limestone) zinazohitajika kuongeza pH.

kiwango kinachohitajika kuongeza pH kinategemea aina ya udongo uliopo kwenye eneo husika, mfano kwenye eneo la ekari moja  ni kama ifuatavyo,

            pH            kichanga       Tifutifu         Mfinyanzi 

          4.0-6.5     1305kg              3175kg           4525kg

Namna ya kushusha pH (alkaline)shambani, kiwango cha sulphur huhitajika kwa kilogram kulingana na ukubwa wa eneo uliopo.

              pH                 Kichanga       Tifutifu          Mfinyanzi

           8.5-6.5             870kg            1175kg            1390kg

     Hii husaidia kuweka uwiano sahihi wa pH kwenye shamba lako, wakati mwingine zao sahihi huchaguliwa kupandwa kulingana na pH iliyopo kwenye udongo wako iwapo pH haitawezwa kurekebishwa kwa wakati huo.

NAMNA YA KUCHUKUA SAMPULI 

(SAMPLE).

Chukua sample ya udongo kutoka sehemu tofauti tofauti ndani ya shamba lako,  kwa kuchimba shimo la urefu wa centimita 20 hadi 25 na hakikisha vyombo vya kuweka sampuli yako ni visafi na vikavu,Baada ya kukusanya sampuli zako zianike juani hadi zikauke vizuri ili ziweze kutoa majibu sahihi, sampuli zenye unyevunyevu mara nyingi hutoa majibu yasiyo sahihi.

Jinsi ya kuchukua sampuli

Baada ya kuchukua sampuli na kuziweka vizuri peleka maabara ya udongo kwa maandalizi ya kupima udongo wako ili kujua virutubisho vyote vilivyomo kwenye udongo. baada ya majibu yote kupatikana ripoti huandaliwa ya majibu ikionyesha viwango vyote vilivyopo kwenye udongo. baada ya hapo ushauri unatolewa kulingana na maji ya udongo wako.

Mfanano wa matokeo baada ya kupima udongo

Je? unahitaji kupimiwa udongo?                   Kampuni yetu ya Holly Green Agric Group Limited ina uzoefu mkubwa wa kupima udongo tuna uzoefu wa zaidi ya miaka 5 katika suala la upimaji wa udongo,kwa uhitaji wa kupima udongo karibu  tunapima udongo na kutoa ushauri wa zao lipi ulime kulingana na majibu ya udongo wako,  Pia tuna andaa ripoti ya majibu na kukupa ushauri wa namna ya kufanya uwiano sawa wa virutubisho vya udongo iwapo vitakuwa vimepungua au kuzidi ili upata uwiano sawa kwa ubora wa  mazao yako.            Gharama za kupima udongo ni shiling TZS 80,000/= kwa sampuli lakini kutokana na udongo kufanana na kutofautiana ni ngumu kuweza kujua gharama ya upimaji kwa hekari kwani unaweza kukuta ndani ya shamba moja hekari mbili zina udongo unaofanana au zaidi , pia hata hekari moja ina udongo aina mbili tofauti . kwa hiyo kama shamba ni kubwa ni vizuri wataalamu wetu kufika na kuangalia mtawanyiko wa udongo na kuweza kutoa gharama za upimaji .

Veronica J. Joseph

BSc Horticulture

Phone:+255766856431

Email:veronicajj94@gmail.com

Share:

Previous Post
WHY WE
Next Post
ONIONS BRINGING

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 5
  • IRRIGATION 1
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited