• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

NJIA NZURI YA KUANDAA UDONGO WA KITALU NA KITALU CHENYEWE

Home / AGRONOMY / NJIA NZURI YA KUANDAA UDONGO WA KITALU NA KITALU CHENYEWE
  • July 20, 2022

Wataalamu ABDUL MKONO (MWL ABUU)  BSc AEA, SUA                      

 a2mkno@gmail.com  0767359818 /

0652359818Eng  OCTAVIAN J LASWAYIRRIGATION AND WATER0763347985/0673000103

 Naitwa KULTHUM kutoka DODOMA kutokana na nakala zako nzuri za kilimo kama hiyo ilopita ya mbolea ningependa kujua jinsi ya kuandaa udongo kwa ajili ya kitalu cha kisasa (Seedling Trays). Kwa ajili ya kusia mbegu zangu za nyanya.MAJIBU: Kuna baadhi ya mazao ambayo kama mkulima huwezi kuyapanda moja kwa moja shambani lazima kwanza uweze kuyaandaa katika kitalu ili yahifadhiwe kwa muda maalumu (Mara nyingi sio chini ya wiki tatu kwa mazao ya matunda na mboga mboga). Kisha kuhamishwa shambani yakiwa na afya. Sasa katika maandalizi ya kuandaa mmea kitaluni zipo njia kuu mbili za kuandaa mmea katika kitalu. Njia hizo ni:-1.  Kitalu cha kisasa

    2.   Kitalu asili

1. KITALU CHA KISASA: Kitalu hichi huandaliwa katika plastiki maalumu ambazo zina matundu (Seedling Trays). Plastiki hizi huwekewa udongo maaulumu katika matundu hayo kisha mbegu huwekwa katika udongo huo kwa ajili ya kukuzwa. Huu udongo huuzwa lakini pia kuna njia maalumu za kuuandaa udongo huo. Na hapa ndo swali lako lilipo.Kuandaa udongo huu unapaswa kuandaa vifaa vifuatavyo:-1.      Udongo2.      Mchanga3.      Samadi4.      Majani yaliyooza (Humus)Udongo unapaswa kuwa mara nne (4) ya mchanga, samadi, na majani yaliyooza (Humus). Kwa mfano: kwa mkulima mwenye mbegu 2500 za nyanya ataanda udongo kilo 30, mchanga kilo 7.5, samadi kilo 7.5 na ,majani yaliyooza kilo 7.5.Mara baada ya kuwa na vifaa hapo juu utachanganya udongo, mchanga, samadi na majani yaliyooza kwa pamoja kisha chukua maji uchanganye mchanganyiko huo. Kiasi cha maji kiwe kidogo kiasi cha kupata tope dogo tu. Kisha baada ya hapo udongo huo utawekwa katika matundu hayo kisha unachukua kifaa kikali na chembamba kama spoku kwa ajili ya kutoboa katika udongo huo ili kupata nafasi ya mbegu ambayo itawekwa na kufukiwa na kiasi cha udongo kilichotolewa. Kwa kawaida udongo unaotolewa ni kidogo tu mfano wa mbegu husika.Baada ya mbegu kuwekwa katika tray hizo itafunikwa na nailoni nyeusi kwa muda wa siku tatu ukiwa unachunguza kama mbegu imeshaota. Ukiona mbegu zishaota ondoa nailoni nyeusi kisha chukua trei hizo uziweke mahali ambapo pana kivuli kama chini ya mti au tengeneza kichanja. Hapa utaendelea kumwagilia maji asubuh na jioni mpaka siku ya kuhamisha. Wiki moja kabla ya uhamisha shambani punguza umwagiliaji na siku ya kuhamisha usimwagilie kabisa ili uweze kuhamisha mmea na udongo wake.KUMBUKA: Umwagiliaji ufanyike pole pole sana kwani ukifanyika haraka waweza kuondoa udongo na siku ya kuhamisha mmea ukahamishwa bila ya udongo wake. Lakini pia ikitokea mkulima amekosea kuchanganya udongo kwa uwiano sahihi nilioelekeza inaweza kupelekea mmea kushindwa kuhamishwa na udongo wake. Lakini pia kama mkulima akishindwa kuandaa udongo huu atapaswa kununua udongo maalumu kwa ajili ya kusia mbegu. Udongo huo pia ni mzuri na utamsaidia mkulima kuhamisha mmea wake shambani ukiwa na udongo.Picha ya kwanza kushoto kitalu cha kisasa kikiwa na udongo uliotengenezwa kwa uwiano nilioelekeza pale juu. Na kulia ni picha ya kitalu cha kisasa.

2. KITALU ASILIA: Kitalu hiki hutumika na asilimia kubwa ya watanzania kutokana na maandalizi yake ni mepesi. Huandaliwa kwa kunyanyua tuta kimo cha sentimeta ishirini. Kisha huwa na upana wa mita mbili na urefu kutokana na idadi ya miche husika. Kisha tuta hilo huandaliwa vifereji ambavyo vitaachana sentimita 20 kuelekea upana ulivyo. Na vifereji hivyoh huwekwa mbolea na kulowanishwa. Kisha mbegu humwagwa katika vifereji hivyo na kufukiwa vyema. Baada ya hapo kitalu choote hufunikwa na matandazo ili kuhifadhi unyevu. Baada ya siku tatu miche ikiwa ishaanza kutoka utaondoa matandazo kisha utaweka kichanja. Baada ya siku 21 au zaidi mmea utakuwa na afya kwa ajili ya kuhamishwa shambani. Hapa utahitajika kupunguza umwagiliaji wiki moja kabla ili kuuandaa mmea kwa ajili ya kuhamishwa shambani. Changamoto kubwa ya kitalu hiki cha asili baadhi yam mea itashindwa kuhamishwa shambani ikiwa na udongo hivyo kupelekea kufa ikiwa shambani. Angalia picha ya kitalu cha asili:-

Wataalamu 

ABDUL MKONO (MWL ABUU)  BSc AEA, SUA                      

 a2mkno@gmail.com  0767359818 0652359818

Eng  OCTAVIAN J LASWAY

0763347985/0673000103

Share:

Previous Post
MWONGOZO WA
Next Post
HATARI VIWAVI

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 5
  • IRRIGATION 1
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited