• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA UFUGAJI WA SAMAKI

Home / POST HARVESTING, / MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA UFUGAJI WA SAMAKI
  • July 20, 2022

Godfrey, Christopher SwayMtaalamu wa samaki kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA.+255752799673/ 0655859810Kwa mahitaji ya ushauri, utengenezaji wa bwawa, utunzaji wa bwawa,uchanganyaji wa chakula, wasiliana nasi•Mfugaji anatakiwa awe na shauku na dhamira ya kweli ya ufugaji.•Kufanya tathmini ya rasilimali alizonazo kwa ajili ya mradi wa ufugaji wa samaki.•Chanzo endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi.•Hulka ya uvumilivu na kuthubutu.•Tathmini ya soko la bidhaa za samaki.•kujipatia maarifa ya msingi ya ufugaji wa samaki

      SIFA ZA ENEO LA KUFUGIA SAMAKI

·Eneo la kufugia samaki linatakiwa liwe na maji ya kutosha kwa mwaka mzima.·Eneo la kufugia samaki linatakiwa liwe na udongo unaoweza kutuamisha maji.·Eneo zuri la kufugia samaki ni kuwa eneo lisiwe na historia ya mafuriko, kwa kuwa mafuriko yakitokea samaki waliokuwa bwawani wataondoka na maji na bwawa litafunikwa na udongo.·Eneo zuri la kufugia samaki ni lile linalofikika kwa urahisi.·Eneo la kufugia samaki pia linatakiwa kuwa ni eneo lenye amani na utulivu na watu wenye kuelewana. ·Kuwa na soko la bidhaa.·kuwa na umiliki wa ardhi wa uhakika.

AINA NA JINSI YA UTENGENEZAJI WA BWAWA LA SAMAKI

Zipo namna mbalimbali za utengenezaji wa bwawa la samaki, kulingana na aina ya bwawa lenyewe, Hali ya uchumi, wingi wa samaki watakaofugwa pamoja na aina ya samaki watakaofugwa.

Zifuatazo ni Aina za mabwawa ya kufugia samaki.

        1.Bwawa la kuchimba udongo bila kujengea “Earthen Pond. 

          

 2. Bwawa la kuchimba udongo na kujengea kwa Matofali, Simenti na Zege.

JINSI YA KUANDAA NA KUPANDIKIZA VIFARANGA AU MBEGU ZA SAMAKI KATIKA BWAWA LAKO.

Kabla ya kusafirisha vifaranga kutoka kwenye bwawa wanaloishi ni vema vikatolewa na kuwekwa kwenye vibwawa vidogo vidogo kwa muda wa kati ya saa 24 hadi 72 (kutegemeana na umbali wa safari) bila chakula.Wakati wa kupandikiza mfugaji anatakiwa akifika asivimwage vifaranga kwenye bwawa bali anatakiwa kuyaruhusu maji yaliyobeba vifaranga yabadilishane ujoto na maji yatakayopokea vifaranga. Hapa mfugaji anatakiwa kuliweka kontena au chombo alichobebea vifaranga kielee kwenye maji anayotaka kufugia kwa muda wa dakika kati ya 30 hadi 35, baada ya hapo chombo kilicho na vifaranga kifunguliwe na kiinamishwe ili maji hayo yaweze kukutana na yale yaliyoandaliwa kwa ajili ya kufugia na hapo ataruhusu vifaranga kuingia wenyewe kwenye bwawa husika.
Iwapo utafika na kuvimwaga vifaranga kwenye bwawa jipya bila kufuata utaratibu huo wa kitaalamu basi tofauti ya ujoto wa maji kati ya chombo kilichosafirishiwa vifaranga na bwawa unaweza kusababisha vifaranga wote kufa kwa muda mfupi, kitaalamu wanasema kuwa vifo vya vifaranga hivyo vinasababishwa na mshituko wa joto.
Jambo lingine la kuzingatia ni kuwa uandaaji na usafirishaji wa vifaranga ni vizuri ukafanywa muda ambao hali ya hewa inakuwa na ubaridi. Muda unaopendekezwa zaidi na wataalamu ni asubuhi au jioni kwa sababu muda huo samaki wanakuwa na uwezo wa kuhimili misukosuko ya safari tofauti na hali ya hewa inapokuwa ya joto.

    UFUGAJI WA SAMAKI WAKATI WA KIANGAZI NA MASIKA

Kimsingi hakuna tofauti kubwa wala athari kubwa sana za ufugaji wa samaki wakati wa kiangazi ukilinganisha na wakati wa masika, tofauti zilizopo ni ndogo ndogo ambazo kitaalamu hazina madhara makubwa kwa mfugaji.Ø ulaji wa chakula wa samaki na ukuaji wao Ø uchafuzi wa maji yanayoingia kwenye mabwawa ya kufugia

    ULISHAJI NA UTUNZAJI WA SAMAKI BWAWANI. 

•Samaki  wapewe chakula angalau mara 2 kwa siku (saa 3-4 asubuhi  na 9-10 jioni) /hewa ya kutosha .•Kuwapa vyakula tofauti kutegemeana na silka ya aina ya samaki unaowafuga.•Kuna samaki wanaofaidika na vyakula vya nyama nyama kama vile kambale na sangara (hawa hawali pumba) na kuna samaki wengine kama sato wanakula vyakula mchanganyiko wa nyama na mboga mboga na wapo wengine wanaokula vyakula vyenye asili ya mimea tu “carps”.
                                 TABIA ZA ULAJI WA SAMAKI1)   Samaki wanaokula nyama, (sangara na kambale).2)   Samaki wanaokula mimea ‘carps’.3)   Samaki wanaokula vyakula mchanganyiko (nyama na mimea) kama perege, sato na mwatiko (samaki wa maji chumvi).
     MUONGOZO WA MAHITAJI YA VIINILISHE VYA           SAMAKI
Wanga  20-25%Mafuta 10-15%Vitamin 1-2%Madini 1-2%Protini  18-45% NB; Maji – hapa ifahamike kuwa wakati tunazungumzia viwango vya maji vinavyohitajika kwa wanyama wengine wafugwao, hitaji la maji kwa samaki ni ubora wa maji anayofugiwa na sio wingi wake.

                                TARATIBU ZA ULISHAJI WA SAMAKI

MASOKO YA SAMAKI

Ø Soko la awali, hili ni soko la moja kwa moja kutoka kwa muuzaji ambaye ni mfugaji kwenda kwa mlaji,Ø Soko la kati, katika soko hili kwa kawaida kunakuwa na mtu wa kati ambaye ananunua samaki kwa mfugaji kwa lengo la kwenda kuwauzia walaji.Ø Soko la kimataifa, hili ni soko linalofanyika nje ya nchi (baina ya nchi moja na nchi nyingine).

Kwa mawasiliano zaidi juu ya ufugaji wa samaki, ushauri, na usimamizi wa kitaalamu

Godfrey, Christopher Sway
Mtaalamu wa samaki kutoka
Chuo kikuu cha Kilimo SUA
+255752799673/0655859810.  

Share:

Previous Post
ONGEZA KIPATO
Next Post
NJIA BORA

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 1
  • IRRIGATION 5
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited