• Call Us+255 676 262757
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Write Emailsales@greenagriculturetz.com

Digital marketing is the component of marketing that uses the Internet and online based digital technologies such as desktop computers, mobile phones and other digital media and platforms to promote products and services.

  • ADDRESS:

    California, TX 70240
  • EMAIL:

    support@validtheme.com
  • PHONE:

    +44-20-7328-4499

Get Subscribed!

Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited
  • Home
  • About
    • Our Company
    • Message From CEO
    • Our Team
    • Our Clients
  • Our Services
    • Farm Planning & Layout
    • Soil Testing and Analysis
    • Irrigation system design and installation
    • Green house design and installation
    • Training and Capacity Building
    • Fish Pond Design and Construction
    • Rainwater Harvesting System Design
    • Post Harvest Technologies
    • Solar Power Equipment and Water System
    • Supplies of Products and Equipments
  • Our Products
  • News & Updates
  • Contacts
  • Request a quote

ONGEZA KIPATO CHAKO MARADUFU KWA KUFUGA SAMAKI AINA YA PEREGE  KIBIASHARA

Home / POST HARVESTING, / ONGEZA KIPATO CHAKO MARADUFU KWA KUFUGA SAMAKI AINA YA PEREGE  KIBIASHARA
  • July 20, 2022

Godfrey, Christopher Sway

Mtaalamu wa samaki kutoka Sokoine University of Agriculture

+255752799673 / 0655859810

Ufugaji samaki ni kazi ya kupanda, kukuza na kutunza samaki katika mabwawa, mito, mifereji au eneo lililotengwa kwa ajili ya ukusanyaji wa maji, (water harvesting ponds) uzio (uliotengenezwa kwa vyuma, nyavu au miti) au eneo lolote ambalo udhibiti wake yako chini ya mamlaka ya mfugaji mwenyewe. Mabwawa  ya samaki hutengenezwa au huchimbwa kwa njia tofauti tofauti, yaweza kuwa ni ya kuchimbwa na watu (japokuwa ya asili pia huweza kutumika) Samaki pia wanaweza kufugwa baharini au ziwani kwa kutumia vizimba (cages) Pia uzio unaweza kuwekwa katika eneo lolote lililo na maji kama ziwa au baharí au chemichemi. Perege /sato /Tilapia wapo wa aina tofauti tofauti kama vile perege wa Mosambique, Perege weusi, perege wa victoria na wale shiranus. Tofauti zao ni ndogo sana na mara nyingi ni vigumu kuwatambua.


Ufugaji samaki kwa kiasi fulani si sawa na ukuaji samaki katika mito, maziwa na bahari. Tofauti iko katika huduma inayotolewa kwa samaki wafugwao na idadi ya samaki wanaopaswa kuwamo ndani ya eneo husika. Samaki waliofugwa huhitaji kulishwa na kuhudumiwa.Ufugaji wa samaki ni sector inayokua kwa kiasi fulani licha ya changamoto zinazo ikabithi sector hii hapa Tanzania. Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakifuga samaki katika mabwawa 
hata kabla ya nchi yetu kupata uhuru. Lakini baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitoa matunzo hafifu kwa kutofahamu vizuri mambo ya kuzingatia katika swala zima la ufugaji wa samaki kiasi cha kufanya mavuno kutokua mazuri na kupelekea sector hii kushuka na kukua kwa kusua sua. Kwa miaka ya karibuni, serikali imetilia mkazo utoaji elimu (ugani) wa ufugaji samaki ili 
kuboresha mafanikio yake. Wasomaji wetu wa makala hii watasaidika kuogeza uelewa zaidi kwenye ufugaji wa samaki.

MWONEKANO WA PEREGE / SATO NA UMBILE LAKE      

Faida za ufugaji samaki

Hizi ni baathi ya faida za ufugaji wa samaki (perege)1.  Chakula bora chenye uto-mwili (protini) muhimu inayohitajika kujenga mwili.2.  Kujipatia kipato baada ya kuuza samaki waliofugwa.3.  Kuboresha kazi nyingine za kilimo kama bustani ya mboga, ufugaji wa ng’ombe, bata, kuku, nguruwe, bustani ya miti, n.k.4.  Huwezesha kutumia rasilimali ambayo isingekuwa ikitumika kama kusingekuwa na ufugaji samaki kama vile eneo la ardhi lenye maji maji, pumba za mahindi na mpunga, na mabaki ya mboga mboga kutoka bustanini kwa kulishia samaki.5.  Eneo la bwawa huwa ni sehemu nzuri ya mapumziko.6. Perege pia wanasoko kubwa hapa Tanzania kwan wanakubalika na watu wote.

Hatua muhimu  kuzingatia katika shughuli za ufugaji samaki

1.     Uchaguzi wa mahala panapofaa kwa ajili ya kuchimba bwawa la samaki.2.     Tathmini ya umbo na ukubwa wa bwawa3.     Uchimbaji wa bwawa.4.     Uingizaji na utoaji wa maji katika bwawa.5.     Uwekaji wa mbolea na (majivu).6.     Upandaji wa vifaranga vya samaki.7.     Ulishaji wa samaki na matunzo mengine bwawani.8.     Uvunaji wa samaki na aina ya nyavu/zana zifaazo kutumika.9.     Uhifadhi wa mbegu kwa ajili ya mzungoko mwingine wa upandaji samaki bwawani.

Vigezo muhimu katika kuboresha uzalishaji 

Joto au ubaridi wa maji katika sehemu husika huweza kuongeza au kupunguza hamu ya ulaji wa samaki na hivyo ukuaji wake. 

  • Chakula cha samaki (cha asili na cha ziada), aina ya chakula na kiasi kinachopatikana. Chakula cha asili ni kama vile planktonik au majani na algae wanaoota kwenye mabwawa.
  • Uwingi wa samaki waliomo bwawani kulinganisha na ukubwa wa bwawa. Hapa lazima wingi wa samaki uendane na ukubwa wa bwawa lenyewe.
  • Ubora wa vifaranga (quality) waliopandwa. Vifaranga wenye ubora mzuri huwa na uwezo wa kukua haraka.Na hapa pia mkulima anaweza kuamua kuchagua mbegu nzuri za jinsia moja (mono sex) au mchanganykio wa jinsia kwa ajili ya kupata mbegu za mzunguko mwingine.

Endelea kusoma makala zetu kila wiki ujue faida kubwa zinazotokana na ufugaji samaki.
Wasiliana nasi kwa ushauri, utengenezaji mabwawa, upatikanaji wa mbegu bora, utengenezaji wa chakula cha samaki, ulishaji wa samaki, na Eneo linalofaa kwa ufugaji wa samaki.

Godfrey, Christopher sway
Mtaalamu wa samaki kutoka
Chuo kikuu cha SUA Morogoro
   +255752799673/ 0655859810.

Share:

Previous Post
KWA MATOKEO
Next Post
MAMBO MUHIMU

Leave a comment

Cancel reply

Recent Post

  • 04 February, 2021KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • 04 February, 2021MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • 04 February, 2021KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Tags

category list

  • AGRONOMY 26
  • IRRIGATION 1
  • IRRIGATION 5
  • POST HARVESTING, 7
  • TECHNOLOGY 5
  • Uncategorized 4
Holly%20Green%20Agric%20Group%20Limited

Our vision centers around the creation and innovation of products and services tailored to benefit farmers. Our aspiration is to transform these offerings from mere business ventures into essential components of the agricultural industry, effectively addressing the fundamental needs of the farming community

Explore

  • Farm Planning and Layout
  • Soil Testing and Analysis
  • Irrigation System Design and Installation
  • Solar Power Equipment and Water System
  • Rainwater Harvesting System Design
  • Fish Pond Design and Construction
  • Post Harvest Technologies
  • Training and capacity Building
  • Green house design and installation

Recent Articles

  • KANUNI ZA KILIMO CHA VITUNGUU.
  • MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI
  • KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Contact Info

ADDRESS:
Headquarter :
Pamba House
Plot No. 97-103
Old Dar es Salaam Rd
P.O. Box 910
Morogoro, Tanzania

Branch :
Nazareti Street
HSE Block T508
Njombe, Tanzania

EMAIL:
sales@greenagriculturetz.com

PHONE :
+255 676 262757
+255 767 102418
+255 763 347985

Copyright 2025 Holly Green Agric Group Limited. All Rights Reserved.

Holly Green Agric Group Limited